Shirika la Misaada la Uingereza lamimina mamilioni Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
166
Reaction score
182
SHIRIKA LA MISAADA LA UINGEREZA LAMIMINA MAMILIONI MWANZA

SHIRIKA la Misaada la nchini Uingereza (DFID) limeanza kutoa misaada nchini, baada ya kuanza kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko mawili jijini Mwanza.

Masoko hayo ni Mirongo (Nyamagana) Kiloleli (Ilemela) ambayo yanafanyiwa maboresho ili kuwezesha wafanyabiashara kuwa na mazingira rafiki ya kufanyia shughuli zao.

Pamoja na ukarabati wa masoko hayo, utakwenda sambamba na ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa na ujenzi wa vyumba vya kunyonyeshea akina mama.

Shirika hilo la misaada, linafanya kazi ya ukarabati wa masoko hayo kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na Watoto (Kivulini) la jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini,Yassin Ally, anasema ukarabati wa masoko hayo pamoja na ujenzi wa vyoo, vyumba vya kunyonyeshea utagharimu kiasi cha Tsh. 218.

Yassin anasema kuwa, ukarabati wa masoko hayo unaokwenda sambamba na ujenzi wa vyumba vya kunyonyeshea akina mama, mitaro ya maji taka, kituo cha daladala Kiloleli na jengo la kufanyia biashara.

Anasema ujenzi wa masoko hayo na mambo mengine, unalenga kuinua uchumi wa wafanyabiashara ndogondogo ambao ni wanawake.

Yassin anaeleza kwamba ujenzi wa stendi na ukarabati wa masoko hayo, yatachukua muda wa miezi mitatu huku akibainisha utakwenda kufufua ndoto za wafanyabiashara wadogo jijini humo.

"Sisi tunaenda kutatua zile changamoto zilizokuwa zinawapa changamoto kubwa, na kipekee zaidi soko hili litakuwa la kimfano Tanzania kwa sababu vitu tunavyoweka hapa ni vya tofauti.

"Chumba kimoja cha kunyonyeshea kitakuwa na eneo maalumu la watoto kupumzika na kuchezea wanapokuwa sokoni," anasema Yassin.

Mkuu was mkoa wa Mwanza, ambaye inaelezwa alifika jana katika masoko hayo kukagua maendeleo ya ukarabati wa masoko hayo na kuwataka wafanyabiashara hao kutumia maeneo hayo kwa tija ili yaweze kuwapunguzia umasikini.

Mongella anafafanua kuwa, ukarabati wa masoko hayo na ujenzi wa vyumba hivyo ni ajenda ya Rais Dk. John Magufuli ambaye anataka kuona watanzania wote wakiondokana na umasikini.

Pia Mongella akawasisitiza wafanyabiashara hao kufanya kazi kwa bidii na kwamba waache mzaha katika biashara zao ili ziweze kuwainua kiuchumi.

Sophia Abdul ni mfanyabiashara katika soko la Kiloleli, anasema ujenzi wa soko hilo utawasaidia kuondokana na changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo za kunyeshewa na mvua.

Anasema endapo ujenzi huo utakamilika (wafanyabiashara) watakuwa katika mazingira mazuri na kwamba hata biashara zao zitakuwa nzuri zaidi na watapata wateja.

Mwisho................
 
Wabongo bado tunajivunia misaada na mikopo

Jr
Kwanza pole kwa ubashiri wako kwenda fyongo😜😂👊💣💥

Kama bado tu maskini kwanini tusijivunie..?
Anaehitaji msaada ni asienacho wacha tufurahie tutalipa ktk namna nyengine yenye vululevulule!!

NB: hata upinzani wanafurahia misaada au hujapata namba yao ya kuwatumia..?😜
 
Tukirejea game ya simba na yanga tu wamepiga zaidi ya pesa hizo na taarifa zingine ni aibu kushobokea manake kesho mtawaita mabeberu. Lakini ingekuwa nyie mngejenga daraja lenye kuwaka taa mkapige picha kama la furahisha tena mnatumia mabilioni hapa ndio ninapoamini kuwa mtu mweusi hawezi pata corona.

Tena hakimu aliyehukumu akina Mbowe ndio kabisa amedhihirisha pasina shaka corona hatutapata Tanzania yeye amekusanya 350 milioni kwa kuhukumu tu.
 
Soko kuu lenyewe wataanza lini kulijenga?
Nasikia "kiongozi" kwenye ziara yake hapa Mwanza, alisema kuwa "ATOE HELA YA KUJENGA SOKO KWANI MCHICHA UNAUZIWA GHOROFANI..."
 
.
Kwanza pole kwa ubashiri wako kwenda fyongo

Kama bado tu maskini kwanini tusijivunie..?
Anaehitaji msaada ni asienacho wacha tufurahie tutalipa ktk namna nyengine yenye vululevulule!!

NB: hata upinzani wanafurahia misaada au hujapata namba yao ya kuwatumia..?
tapatalk_1584028848206.jpeg

Jr
 
Back
Top Bottom