Shirika la Kinnapa lapata bodi mpya 2019-2023

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Kinnapa ni Shirika lisilo la Kiserikali ambalo makao makuu yake yako Wilaya Kiteto mkoani Manyara. Shirika linafanya kazi ya ushawishi na utetezi, na pia linachangia upatikanaji wa huduma za jamii kama vile maji, elimu, matumizi bora ya ardhi nk

Shirika linapata viongozi wake kila baada ya miaka mitatu hivyo mwaka huu tena limepata viongozi wapya. Waliochaguliwa kuongoza shirika hilo ni pamoja na Alais Taleki Nangoro kuwa mwenyekiti, Sekemi Sakana kuwa mweka hazina

Wengine waliochaguliwa ni Athumani msimbazi kundi la wakulima, wafugaji ni Yohana Lematawa, na kundi la vijana ni Ibrahimu Ole Mario. Mratibu wa shirika hilo, Abraham Akilimali alisema, uchaguzi huo umetokana na takwa la kisheria ambalo kila baada ya miaka mitatu hufanyika

Mwenyekiti mpya wa shirika hilo alaisi Nangoro, alisema shirika litaendelea kutimiza malengo yake chini ya utawala wake kwa mujibu wa katiba yao. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, aliwaambia wajumbe hao kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na shirika hilo na kuwataka waendelee kiisaidia Serikali

Nao baadhi ya wajumbe akiwemo Athumani Msimbazi aliyechaguliwa alisema, atatumia elimu yake kuhakikisha shirika linatimiza malengo tarajiwa
 
Back
Top Bottom