Shirika la Afya duniani: Wakunga milioni 9 bado wanahitajika

Shirika la Afya duniani: Wakunga milioni 9 bado wanahitajika

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,844


Dunia itahitaji ongezeko la wauguzi na wakunga milioni 9 ili kutimiza ahadi ya kutoa huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030. Haya yamethibitishwa na Shirika Afya ulimwenguni WHO

WHO na wadau watautumia mwaka huu wa 2020 kupigia upatu uwekezaji katika wahudumu hao muhimu wa afya

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dk. Tedross Adhamon Ghebreyesus alisema “wauguzi na wakunga ni uti wa mgongo wa kila mfumo wa afya na mwaka 2020 tunatoa wito kwa nchi zote kuwekeza kwa wauguzi na wakunga kama sehemu ya ahadi ya huduma za afya kwa wote.”



Dk Teodros alisema kuwa mwaka 2020 ni “Mwaka wa wauguzi na wakunga” na ni maadhimisho ya miaka 1000 tangu kuzaliwa kwa Florence Nightngale muasisi wa uuguzi.
 
Huku kwetu tuna upungufu katika kila kada,Madaktari wa kawaida, wa usingizi,wakunga,madaktari bingwa,madaktari wa watoto nk,sijui tuanze na lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom