Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,279
=====
Shinyanga.Kutokana na ukame kuathiri maeneo mengi ya nchi,wabunge wawili mkoani Shinyanga, wamevunja ukimya kuhusu upungufu wa chakula wakiwataka watendaji wasiogope kutumbuliwa kwa kusema ukweli.
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Stephen Masele wa Shinyanga Mjini, kwa nyakati tofauti walizungumzia suala hilo wiki hii.
Akizungumza wakati akipokea tani sita za mbegu ya mtama wiki hii kutoka Ushirika waIbuka, Maige alisema licha ya Serikali kuzuia kutangaza uwapo wa njaa, maeneo mengi jimbo ni mwake yanakabiliwa na ukame unaoashiria kuna upungufu mkubwa wa chakula.
“Hali ya chakula jimboni kwangu ni mbaya na tayari nimewasiliana na Ofisi ya Waziri wa Chakula ili watuwezeshe kupata chakula cha bei nafuu watakachouziwa wananchi,” alisema Maige.
Katika tukio ingine, Masele aliwataka viongozi waliochaguli wa na wananchi wakiwamo wabunge na madiwani kutoogopa kusema ukweli kama wanakabiliwa na njaa kwenye maeneo yao.
Akiwa ziarani jimboni humo, aliitaka Serikali kutambua kuwa wananchi wana njaa, hivyo wapatiwe chakula kitakachouzwa kwa bei nafuu.