MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,093
Watanzania ni wepesi wa kusahau, wanasahau mapema mithili ya maisha ya nzi Mwaka 2017 kulikuwa na ukame mkali hadi kupungua kwa chakula kabisa hakuna aliyethubutu kusema hata kidogo. Watanzania ni wanafiki wa kiwango cha SGR.
Wamesahau Magufuli akiwa Kwenye ziara mkoani Simiyu wakulima walipomlilia njaa aliwajibu yeye si Baba yao wakatafute chakula wanapojua wao.
Mwaka ule ni Baraza la Maaskofu lilithubutu kuweka wazi juu ya baa la njaa kupitia taarifa ya baraza la maaskofu wa kanisa Katoliki.
Kutoka kwa Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania katika barua yake iliyotiwa mkwaju tarehe 13 Januari 2017.
Tarcisius Ngalalekumtwa ndio Askofu wa Kanisa Katoliki ambae aliiongoza TEC kama Rais na haikuwahi kuyumbishwa chini ya mamlaka yake hata siku moja. Kumbuka waraka wa TEC kuhusu mauaji ya Kibiti na kuhusu haki za binadamu.
Watanzania wana kasumba ya unafiki inatutesa hadi leo Mwaka 2017 nchi ilikumbwa na ukame mkali hatukupewa taarifa kila mtu alikufa na njaa yake, maji na Umeme vilikuwa vya tabu kwakuwa tunasahau leo tumeubeba ukasuku.
Ni kanisa Katoliki pekee lilisimama kuisema Serikali itangaze juu ya hali ya Ukame. Iweje leo muishambulie Serikali inayowaambia ukweli juu ya upungufu wa mvua?
Hakuna Serikali inayopenda watu wakae gizani, wafe na njaa pamoja na kiu hakuna hiyo Serikali. Mabadiliko ya tabia nchi yanatuadhibu sote tujipange kama Wananchi kulinda na kuyatunza mazingira ukikosa maji leo kesho amka upande mti mmoja hata wa mwarubaini.