PreGE2025 Shinyanga: Viongozi 50 wa NCCR Mageuzi wahamia Alliance for Democratic Change (ADC)

PreGE2025 Shinyanga: Viongozi 50 wa NCCR Mageuzi wahamia Alliance for Democratic Change (ADC)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,410
Reaction score
4,988
Viongozi 50 wa majimbo, wilaya na kata wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Shinyanga wamehamia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) huku wakiweka wazi sababu zilizowahamisha.

Akizungumza mkoani Shinyanga wakati wa kuwapokea viongozi hao Mwenyekiti wa ADC Taifa, Shaban Itutu mbali na kuwapongeza, ametoa wito kwa viongozi, wanachama na wananchi wa kawaida walio tayari kujiunga na chama hicho wafanye hivyo kabla ya kuingia kwenye uchaguzi.

Dismas Thomas, aliyekuwa Katibu wa NCCR Mageuzi Jimbo la Msalala akizungumza mara baada ya kupokelewa kwa viongozi hao amedai chama cha NCCR Mageuzi kinaendeshwa katika mfumo usiokuwa mzuri, hali iliyowafanya kuhamia ADC ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Akiunga mkono hoja hiyo aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Jimbo la Kishapu, Joyce Masanja amedai pia ukosefu wa huduma nzuri ndani ya chama hicho imemfanya ahamie ADC.

"Changamoto iliyonitoa kule huduma haikuwa nzuri ndio maana nimeona nirudi huku nimeona hiki chama kitatutoa kutupeleka hatua nyingine," amesema Masanja

Naye Katibu wa NCCR Mageuzi Jimbo la Ushetu, William Lucas amesema baada ya kugundua chama hicho kinaendeshwa pasina kufuata matakwa ya chama na wanachama, ikamfanya atafute chama kingine anachoamini kitaleta ukombozi.

Kamishina wa ADC Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Khalid Saganda ameahidi ushirikiano kwa viongozi hao waliohamia katika chama hicho.

"Tunatoka nyumba ya zamani tunakuja kukaribishwa nyumba mpya kwa maana kwamba tunatoka NCCR Mageuzi sasa tunakuja ADC ambapo ndipo inapopatikana dira ya mabadiliko," amesema Dkt. Saganda

 
Mikokoteni yote hiyo inaelekea machinjioni NCCR ADC ndio maana CHADEMA tunasema NO REFORMS NO ELECTION.
 
No reform no elections igusie hili suala la kutaja VIONGOZI WA CHAMA Fulani. ............wamehamia chama Fulani. .....


Utaratibu mpya utumike habari isome wanachama wapya wajiunga na chama Fulani .kwanini kudharirishana mchana kweupe pasipo sababu za msingi .Kama Una hama chama si uame Kwa Amani na si mpaka kuita press Ati tunajitoa ...wewe Kama unajitoa jitoe Tu .



No reform no elections.💪
 
Back
Top Bottom