SHINYANGA: Mtoto afariki kwa kukanyagwa na gari akiwa nyumbani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na gari wakati dereva akirudisha gari lake nyuma bila kuchukua tahadhari.

Tukio hilo limetokea Muda wa usiku kwao na mtoto huyo katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.

Kwa Mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo na kata hiyo,David Nkulila amesema mtoto huyo amekanyagwa na gari hilo linalodaiwa kuwa ni la serikali nyumbani kwao.
 
RIP mtoto...
Hii inakumbusha umakini kwa madereva...
Pia kwa wazazi...
Ukipita uswahilini unajiuliza maswali mengi sana...mtoto anatambaa barabarani mama anaendelea na shughuli zake...
Mtoto anatakiwa kuwa machoni pa walezi muda wote...
Ni Mungu tu anayewalinda...
 
Unlike nchi zilizoendelea huku kwetu malezi ya watoto ni ya kushangaza sana...
Kuna siku niliona baba amepakia mwanae kwenye pikipiki (nadhani ni yake) asubui anampeleka shule nilitamani nimkamate lakini mi si traffic.
Yule mtoto alikuwa amemshikilia baba yake lakini amesinzia...
Kwa nini kusiwe na sheria ya kuzui kupakia watoto kwenye pikipiki?
 
Ni vyema sana kufunga kamera za nyuma, mbali na kugonga watoto kuna visiki vidogovidogo ambavyo huharibu sana bampa la nyuma! Cha ajabu wanaofunga kamera huwa tunawaaita ma-LEANER!
 
RIP mtoto...
Hii inakumbusha umakini kwa madereva...
Pia kwa wazazi...
Ukipita uswahilini unajiuliza maswali mengi sana...mtoto anatambaa barabarani mama anaendelea na shughuli zake...
Mtoto anatakiwa kuwa machoni pa walezi muda wote...
Ni Mungu tu anayewalinda...
Na kweli ni mungu tuu ndo anaewalinda
 
RIP mtoto, aisee mimi huwa nachukua tahadhari sana kwanza kabla hujawasha gari kuondoka hakikisha watoto wote wapo ndani, kabla sijaingia getini nashuka kwanza kupitia geti dogo ili kuhakikisha watoto wote wamefungiwa ndani, kabla sijamfungulia geti mtu kuingia ndani nahakikisha watoto wote wamefungiwa ndani. Nimesikitika sana. Watu wazima tuchukue tahadhari kulinda watoto wetu.
 
Unlike nchi zilizoendelea huku kwetu malezi ya watoto ni ya kushangaza sana...
Kuna siku niliona baba amepakia mwanae kwenye pikipiki (nadhani ni yake) asubui anampeleka shule nilitamani nimkamate lakini mi si traffic.
Yule mtoto alikuwa amemshikilia baba yake lakini amesinzia...
Kwa nini kusiwe na sheria ya kuzui kupakia watoto kwenye pikipiki?
Una hoja nzuri, kupakia watoto wadogo kwenye pkpk ni hatari sana, wanasinzia na hawana uwezo na nguvu za kujishikikia vzr.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa mwaka mmoja anakuwa nje usiku............. Dah poleni wafiwa. RIP mtoto
 
Back
Top Bottom