Shinyanga: Mkemia Mkuu asema maji na tope la bwawa la Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) havina madhara kwa binadamu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa, Musa Kuzumila amesema kuwa maji na tope la bwawa la Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) havina madhara yoyote hivyo wananchi wanaruhusiwa kutumia na kunywesha mifugo kama kawaida.

Maji na tope hilo yametokana na bwawa la majitaka la mgodi huo unaomilikiwa na kampuni hiyo (asilimia 75) na Serikali (asilimia 25) kupasuka Novemba 7 mwaka huu na kutiririsha maji hayo yenye tope kwenye makazi ya watu.

Akitoa taarifa ya uchunguzi leo Jumamosi Novemba 12, 2022 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kuzumila amesema baada ya kufanya upimaji walibaini kuwa maji na tope hilo havina madhara ya aina yeyote.

"Tulianza upimaji wa sampuli Novemba 9 baada ya tukio hili kutokea tulipima maji na tope ambapo tulichukua maji magharibi mwa bwawa la almas na upande wa kwenye vijiji vilivyoathirika, hivyo tulibaini tope na maji hayana kemikali ya aina yoyote, maji hayo yapo salama hivyo tunawaomba wananchi wasiwe na hofu tena,"amesema Kuzumila.

Kwa upande wake meneja wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ziwa Mwanza, Jarome Kayombo amesema kuna uchunguzi mbalimbali umefanyika kuhusiana na bwawa hilo kupasuka ofisi ya mkemia wamepima wameona maji hayo hayana madhara kwa wananchi na kwa wanyama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amesema baada ya bwawa kupasuka maji yakatiririka wananchi walishindwa kutumia maji kwa kuhofia yana madhara, lakini vipimo vimeonyesha maji haya ni salama, hivyo wanatakiwa kutumia bila wasiwasi.

Pia soma: Dokezo - Uchafuzi Wa Mazingira: Mgodi wa almasi Shinyanga
 
Almas wanachoronga miamba hakuna kemikali zinazotumika kwenye almas kama ilivyo uchenjuajinwa dhahabu.

#MaendeleoHayanaChama
Hata kama lingekuwa bwawa,la kuhifadhia maji ya kuchenjulia mabaki ya dhahabu,usitegemee wataalam hao wakuambie kuwa ni hatari kwa matumizi ya binadamu,ili kuogopa taharuki kwa wananchi,Hii ndio Africa bnana!!wanafahamu hata kama kuna madhara ni yale ya pole pole sana.Itokee leo hii taasisi ya kimataifa iseme kuwa ikafanye uchunguzi wake uone kitakacho tokea,kwanza huwezi pewa ruhusa.
 
Hawa watu wamekimbia makazi yao, yani vijiji kadhaa vimeathirika... kijiji kimoja kina kaya zisizo pungua 250, hivyo ni kaya nyingi zenye kubeba watu wengi...

Wame kimbia kwa taharuki, wame kimbia kwa kuokoa uhai na usalama wao

Kwanza eneo ambalo ni sehemu ya ukuzaji uchumi wa kaya zao lime vamiwa na tope na maji ambayo sio ya mvua, sio ya dawasa Au morowasa Au wasa wasa zingine bali ni maji ya mgodi

Hawa watu wa mgodi wana takiwa kuvilipa hivi vijiji hawa hawa wana kaya hizi kwa kilicho tokea

Hawa wakipata mtetezi ata mashirika binafsi kama wamasai basi wata nufaika na wata heshimiwa ktk maeneo yao

kule mara kila baada ya Muda fulani tuna sikia maji kutoka migodini yame Pelekwa ktk mito na hayana madhara lakini sizani...
 
Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa, Musa Kuzumila amesema kuwa maji na tope la bwawa la Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) havina madhara yoyote hivyo wananchi wanaruhusiwa kutumia na kunywesha mifugo kama kawaida.

Maji na tope hilo yametokana na bwawa la majitaka la mgodi huo unaomilikiwa na kampuni hiyo (asilimia 75) na Serikali (asilimia 25) kupasuka Novemba 7 mwaka huu na kutiririsha maji hayo yenye tope kwenye makazi ya watu.

Akitoa taarifa ya uchunguzi leo Jumamosi Novemba 12, 2022 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kuzumila amesema baada ya kufanya upimaji walibaini kuwa maji na tope hilo havina madhara ya aina yeyote.

"Tulianza upimaji wa sampuli Novemba 9 baada ya tukio hili kutokea tulipima maji na tope ambapo tulichukua maji magharibi mwa bwawa la almas na upande wa kwenye vijiji vilivyoathirika, hivyo tulibaini tope na maji hayana kemikali ya aina yoyote, maji hayo yapo salama hivyo tunawaomba wananchi wasiwe na hofu tena,"amesema Kuzumila.

Kwa upande wake meneja wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ziwa Mwanza, Jarome Kayombo amesema kuna uchunguzi mbalimbali umefanyika kuhusiana na bwawa hilo kupasuka ofisi ya mkemia wamepima wameona maji hayo hayana madhara kwa wananchi na kwa wanyama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amesema baada ya bwawa kupasuka maji yakatiririka wananchi walishindwa kutumia maji kwa kuhofia yana madhara, lakini vipimo vimeonyesha maji haya ni salama, hivyo wanatakiwa kutumia bila wasiwasi.

Pia soma: Dokezo - Uchafuzi Wa Mazingira: Mgodi wa almasi Shinyanga
Hawa Binadamu sio wa kuwaamini.... Ni kama yale ya Mara tuliambiwa ni Kinyesi cha ng'ombe
 
Back
Top Bottom