Shinikizo la juu la damu (High blood Pressure) Fahamu chanzo, kinga na tiba ya tatizo hili

pole kwa tatizo linalokusumbua, kwa maelezo uliyotoa naomba nikushauri kama ifuatavyo:

1. Tatizo la High blood Pressure halitibiki ,kinachofanyika ni kutumia dawa ili kuzuia uharibifu wa viungo vingine kama figo,moyo,macho na ubongo ( Stroke),

2.NI VIZURI UKIFAHAMU KUWA UNAWEZA KUTUMIA DAWA KWA MAISHA YAKO YOTE, ni aina gani ya dawa na utatumia kwa utaratibu gani hili daktari wako atakueleza,ila kwa kawaida unaweza kubadilishiwa dawa na kufanya dosage adjustments mara kadhaa.

3. Jenga tabia ya kupima Pressure yako mara kwa mara,Siku hizi kuna digital Blood Pressure monitors nyingi zinapatikana kirahisi madukani,hii itakusaidia ku monitor na kujua ufanisi wa dawa unazotumia,Nakushauri utafute daktari bingwa wa magonjwa ya ndani (Physician) uwe unaenda Clinic kwake angalau mara moja kila mwezi.

4. Uwiano wa uzito na urefu wako hauko sawa ,kwa vipimo ulivyosema ,Uwiano (Body Mass Index) Yako ni 32, Normal Range ni 18 hadi 24! kwa sababu huwezi kuongeza urefu,inabidi upunguze uzito hadi ubaki na kilo zisizozidi 70 ili uwiano / BMI iwe sawa,Hii inawezekana kwa kupangilia mlo wako,unaweza kutafuta dietitician atakusaidia.

5. Ni vizuri ukifanya vipimo vya figo kwa maana ya Renal Profile / Renal Function test na usisahau Renal Ultrasound, Kuna uhusiano mkubwa wa matatizo ya Figo na High Blood Pressure.

NASISITIZA HILI TATIZO HALITIBIKI ILA ZINGATIA SANA USHAURI NA MAELEKEZO YA DAKTARI ILI KUEPUKA FURTHER COMPLICATIONS ( END ORGAN DAMAGE ).
 
pole kwa tatizo linalokusumbua, kwa maelezo uliyotoa naomba nikushauri kama ifuatavyo:

1. Tatizo la High blood Pressure halitibiki ,kinachofanyika ni kutumia dawa ili kuzuia uharibifu wa viungo vingine kama figo,moyo,macho na ubongo ( Stroke)...
Asante sana ndugu this professional adv. Naenda kuonana na physician this week
 
Punguzeni kutumia Madawa ya hospitalini yana sumu na mdahra kwa binadamu tumieni vyakula alivyotuletea Mwenyeezi Mungu muumba havina madhara kwa binadamu na pia ni tiba kwa binadamu. Tumieni kwa wingi wenye Maradhi ya Presha ya kupanda hivyo vyakula nilivyoweka hapo juu vitawasaidia kuondoka na hiyo Presha ya kupanda au kwa lugha ya kiingereza ni Hypertension or high blood pressure ugonjwa unao uwa haraka kwa binadamu asanteni.
kama mtu ameanza dawa za hospital lets say ametumia sikumbili anaweza acha na akabadili lifestyle na pengine kula dawa za asili?
 
Aisee hongera sana mkuu naona wewe ulikutana na mshauri / daktari mzuri ulipoenda kupima mara ya kwanza, nahisi na mimi ningekutana na ushauri mzuri nisingetumia dawa.

Manake ile nimeenda kuchekiwa na kuonekana kama presha iko juu yaaani hapo hapo wakanianzishia dawa kuja kuulizia ndo naaambiwa huruhusiwi kuacha dawa.

Duh
uliuliza baada ya muda gani tangu uanze matumizi ya dawa?
 
Mwaka 2018 nadhani Dec nilikwenda Hospital moja pale jijini Arusha nikiwa naumwa kichwa, baada ya kugika mapokezi nilifanyiwa vipimo vya awali, ikiwa ni pamoja na kupimwa uzito, urefu na BP.

Muuguzi baada yabkypima pressure nilimnote ameshtula sana, akaniukiza kama nina historia ya pressure nilijibu hapana na ndio ulikuwa ukweli. Ila vipimo pale vilionesha nadhani 195/90 kama niko sawa.

Baadae niliingia kwa Dr. Aliniuliza maswali hasa life style yangu nilimjibu vema baadae ali conclude kwa kunishairi nibadilishe namna ninaishi maisha yangu.

Baada ya siku kadhaa nilimchek rafiki yangu ambaye ni Daktari Bigwa tulipiga story nyingi khs Style ya Maisha. Kitu kilichonishtua ninkuwa endapo nitazembea kubadili maisha basi nikianza kunywa dawa ndo itakuwa hivyo katika Maisha yangu yote i real got scared!

Kuanzia tarehe 12 Jan 2019 nilianza mazoezi ya kukimbia (Jogging) Km 1.5 nikizidi kukuwa kimazoezi na hadi Dec 2019, baadae nikajuunga na Jogging club ya Arusha Runners na target ikazidinkukuwa kutoka 10Km kwa mwezi to 20 hadoli 40Km.

Baadae nilipata uhamisho wa kazi kuja Dar, aisee huku nilipata hamasa sana na nimekuwa sana kimazoezi kiasi cha kukimbia 200KM kwa mwezi na na enjoy kabisa sihisi kama napata maumivu.

INSPIRATIONAL
1. Nimeandika hivi kwa sababu nimeona nimefanikiwa kabisa kutokomeza Pressure ambayo ilitishia maisha yangu, nimefanikiwa kupunguza Kg zangu kutoka 86 hadi 60.6Kg as today 16.08.2020 (nimepuma pale kwenye CRDB Marathon) pressure ipo normal, sukari ilikuwa 3.8 (fasting) nilikuwa sijala kitu. BMI iko 22.8 (very good) kuna jamaa nikikutana nao wananiuliza nimefanyeje nimepungua hv au naumwa, huwa nawaonea huruma sana maana najua wao ndo wagonjwa.

2. Zaidi kila nguo inanikaa na nipo slim sana no kitambi tena yaani kiujumla nimebadilika kabisa (Positevely).

3. Sijawahi tumia dawa yyt ya pressure wala dawa yyt ya kupunguza mwili.

4. Normaly napima Pressure kila mwezi lkn each time nikipima pressure inakuwa normal zaidi ya mwaka 1 na nusu.

5. Utaratibu wangu wa kula ni full despeline, (Wanga kidogo sana, wali nakula kwa nadra sana say mara 2 au 1 kwa mwezi, red meat kwa nadra sana.

6. Nimejiwekea target ya kukimbia km 50 kwa week, 200 kwa mwezi.

7. Nimejiunga na Club mbalimbali ya Jogging ili kuwa inspired na kuwa na nidhamu na company ya mazoezi.

8. Niliacha kunywa kitu inaitwa beer kwa muda wote, i take only wine na Gin kidogo sana.

9. Usiku sina utaratibu kwa kula chakula aina yyt isipokuwa matunda au kunywa mtindi pekee.

10. Nimekuwa balozi mzuri wa kuhamasisha friends, relatives na wengine kushiriki mazoeziwalati mwingine hata pacer kama.atataka tukimbie wote. Marafiki zangu nimewaaomba kama wanahitaji urafiki mzuri na mm basi tuungane tufanye mazoezi (Matibabu yatokanayo na pressure ni gharama sana)

Naomba kuwa encourage kila jambo linawezeka ni maamuzi na kuyasimamia hayo maamuzi
Hongera mkuu
 
Back
Top Bottom