Shindano hili linasemwa ni kubwa na la kidunia, mbona mataifa ya uarabuni hayana mwakilishi hapa?

Shindano hili linasemwa ni kubwa na la kidunia, mbona mataifa ya uarabuni hayana mwakilishi hapa?

Siri yangu

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2023
Posts
1,847
Reaction score
3,746
Vijana 18 kutoka nchi mbalimbali watakaoshiriki mashindano makubwa ya Qurani yanayohusisha mabara yote duniani wametambulishwa leo Ijumaa, Februari 27, kwa waumini waliosali katika Msikiti wa Jamiul Nurul Hikma.

Mashindano hayo, yaliyozinduliwa Februari 1, 2026, na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa Machi 1, 2026, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Baadhi ya nchi zinazoshiriki mashindano hayo, yanayoaminika kuwa makubwa kuliko yote duniani ni Canada, Mexico, Barbados, Guyana, Sweden, Ujerumani, Uingereza, New Zealand, Australia, Indonesia na Kazakhstan.

Kwa Bara la Afrika, washiriki wanatoka Reunion, Zambia, Uganda, Kenya na nchi nyingine, huku Tanzania ikipeleka washiriki watatu kama mwenyeji.

Hata hivyo, Mshiriki kutoka Guyana hakutambulishwa, ikielezwa yupo nchini lakini alipata dharura.

Vijana hao wanashiriki mashindano baada ya kuhifadhi Qurani yote yenye juzuu 30, sura 114 na aya 6,236. Wana umri kati ya miaka 13 na 25, mdogo kabisa akiwa Abdulrahman Yassin kutoka Uganda mwenye umri wa miaka 13, huku wenye umri wa miaka 25 wakiwa wawili: Shueyb Mohamed Shafie Hassan kutoka Sweden na Hijja Nassor Hijja kutoka Zanzibar.

Tangu mashindano hayo yazinduliwe Februari 1, wakazi wa Dar es Salaam, Zanzibar na mikoa mingine wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria ili kuwasikiliza vijana hao wakionyesha umahiri wao katika kuhifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Mshindi wa kwanza wa mashindano ambayo mdhamini wake mkuu ni PBZ Bank Ikhlas, atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30.
56702.jpg

Wakuu mimi sio muumini sana wa upande wa maswala ya Dini ila nimesoma hili chapisho ni kama sijalielewa au wenzangu naomba mnieleweshe hadi Sweden wametoa muwakili ila Saudiarabia hakuna mwakilishi kulikoni wakati shindano hili ni kubwa ina inasemekana ni la kidunia na nchi nyingi zimeshiriki na mbona nchi zilizo shiriki ni nchi zenye wakristo wengi zaidi tena walokole haswa
 
Huu ni uchuro wa kidini! Wanahimizana misikitini waujaze uwanja kuliko simba na yanga ionekane dini hiyo inapendwa na ina waumini wengi! Ni propaganda tupu za udini. Upande ule mwingine mwamposa tu peke yake anaujaza uwanja pomoni bila madhehebu mengine. Imagine upande wa pili kwa ujumla wao wahimizane kuhudhuria tukio lao hapo, si utajaza viwanja vitano! Eti mashindano! Hayo mashindano yako chini ya idara gani ya serikali?
 
Back
Top Bottom