Shinda zaidi na sportpesa promotion launch

Shinda zaidi na sportpesa promotion launch

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
203
Reaction score
84

Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Ndugu Tarimba Abbas akizungumzia promosheni mpya iliyozinduliwa na kampuni hiyo ijulikanayo kama SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA, pembeni ni Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya akifuatiwa na Mkurugenzi wa kampuni inayosambaza bajaji Tanzania Ndugu Venkatesh K..


KAMPUNI ya kubashiri michezo nchini ya Sportspesa imezindua rasmi promosheni ya kuinua watu maisha yao hasa kiuchumi inayokwenda kwa jina la Shinda zaidi na Sportspesa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Tarimba Abbas amesema kampuni hiyo inaendesha shindano hilo kwa wateja wake ikiwa ni mara ya pili.

Ambapo kwa mwaka jana ilitoa takribani bajaj 100 kwa washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini waliobuka washindi.


Meza kuu ni kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka Simba, akifuatiwa na Bwana Salum Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa mashindano TFF, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas,Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya, Mkurugenzi wa Kampuni ya SunBeam Venkatesh K, Mkurugenzi wa klabu ya Singida United Festo Sanga pamoja na Katibu wa Yanga Omary Kaaya..

Pia Tarimba amesema lengo la shindano hilo limejikita zaidi kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania kwani washindi wamekua wakishinda zawadi mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingne zinawasaidia kujiongea kipato. Ametoa rai kwa wateja kutumia fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani promosheni hiyo kila mmoja anayo nafasi ya kuwa mshindi na kufafanua shindano hilo linaambatana sana na wapenzi wa mpira wa miguu.Kwa upande wa Submean Auto Limited Venkatesh Bussiness ambao ni wasambazaji wa Bajaji RE nchini wametoa waranti kwa miezi 12 bajaj za watakaoshinda ili kuonesha imani kwa bidhaa hizo.Pia wamewaomba watanzania kubashiri kupitia Sportpesa ili waweze kushinda hasa kwa kuzingatia kampuni hiyo inaongoza kwa Afrika Mashariki.

Zoezi la ufunguzi rasmi wa promosheni ukiongoza na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Tanzania Bwana Pavel Slavkov na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Ndugu Tarimba Abbas..


Wakati huohuo Meneja Uhusiano wa Sportspesa Sabrina Msuya amefafanua jinsi ya kushiriki Kwenye promosheni ya Sindano hilo.
Msuya amesema kwa promosheni iliyopita ilifika mikoa 23 ya Tanzania na kwa kila aliyewekea ubashiri wake alipata nafasi ya kujishindia pesa taslimu,jezi na safari ya kwenda Uingereza ,Bajaji ni fursa peke kwa sasa kubashiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom