KWELI Shimo linaloendelea kuwaka kwa Zaidi ya miaka 50

KWELI Shimo linaloendelea kuwaka kwa Zaidi ya miaka 50

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
1773731053293.png
 
Tunachokijua
Katika Jangwa la Karakum nchini Turkmenistan na Si Libya kama ambavyo imeelezwa katika chapisho Facebook, kuna shimo maarufu linalojulikana kama Darvaza Gas Crater, ambalo mara nyingi huitwa “Door to Hell” au “Gates of Hell”.

Inaelezwa kuwa Shimo hilo lilitokea mwaka 1971 baada ya wataalamu wa jiolojia wa Kisovieti kufanya uchimbaji wa kutafuta gesi asilia katika eneo hilo. Wakati wa uchimbaji huo, ardhi iliporomoka na kusababisha kutokea kwa shimo kubwa lililokuwa likitoa gesi ya methane kutoka chini ya ardhi.

Ili kuzuia kuenea kwa gesi hiyo ambayo ingeweza kuwa hatari kwa mazingira na viumbe hai, wataalamu waliamua kuwasha moto gesi hiyo wakiamini kwamba ingeungua na kuisha ndani ya muda mfupi. Hata hivyo, moto huo haukuzima kama ilivyotarajiwa, na umeendelea kuwaka kwa zaidi ya miaka 50 hadi leo.

Shimo hilo lina kipenyo cha takribani mita 60 hadi 70 na kina cha takribani mita 20 hadi 30. Usiku, mwanga wa moto unaowaka ndani ya shimo hilo huonekana kwa mbali na kuvutia watalii pamoja na watafiti kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Licha ya kuwa kivutio cha kipekee cha utalii na utafiti wa kisayansi, wataalamu wa mazingira wanaeleza kuwa kuendelea kuwaka kwa gesi ya methane kuna athari kwa mazingira, kwani methane ni moja ya gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani. Kwa sababu hiyo, kumekuwa na mijadala ya mara kwa mara kuhusu uwezekano wa kuuzima moto huo katika siku zijazo.​

Attachments

  • Kdabepq48thhum3yjnbCeM-970-80.jpg.webp
    Kdabepq48thhum3yjnbCeM-970-80.jpg.webp
    44.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom