shillingi yazidi kuporomoka

Mmmh hiyo noma me naona malawi na tanzania ngoma droo maliwa saiz dollar inanunuliwa 230 kutoka 180 mwezi wa tatu!
 
wakuu tatizo la kupanda kwa dola na kushuka kwa shilingi linasababishwa na uagizwaji wa mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme hivyo yamesababisha mahitji makubwa ya ziada katika sekta hii
 
Mkuu,

Majuzi katika mkutano mmoja Ben Benarnke alisema there is little that the Central bank can do to save the country economy. Monetary policy bila ya kuwapo kwa sound fiscal policy ni vigumu sana kuokoa uchumi. Benki kuu itajitahidi kuzuia kuporomoka kwa shillingi kwa njia mbali mbali kama kupunguza pesa za kutoka kwenye mzunguko wa fedha, kuingiza fedha zaidi za kigeni nyingi katika mzunguko nk. But Shida ya monetary policy ni kwamba ni measures za muda mfupi kuokoa uchumi. Serikali inabidi ijitahidi kuokoa uchumi wa nchi kuanguka kwa kutatua tatizo la umeme, ufisadi, dollarisation nk. Bila ya strong fiscal policy BOT itabakia kama bubu kwani ikiingiza pesa zaidi katika mzunguko zitashusha thamani za fedha za kigeni kwa muda mfupi lakini baada ya miezi miwili thamani ya dollar itazidi mara mbili ya ilivyokuwa mwanzo na kuzidisha ugumu wa maisha.

Tatizo moja ya watu kama Mdondoaji ni kujaribu kutaka kutatua matatizo yetu kwa kutumia/kuiga jinsi nchi kama marekani inavyotatua matatizo yao ya uchumi na ndio maana wanaquote Ben Barnake anasema nini na kuiga policy prescription zao. Uchumi wa marekani na uchumi wa Tanzania ni tofauti hivyo ni juu ya BOT kutumia njia za kuthibiti mfumuko wa bei relevant to our situation; kwani ikumbukwe kuwa exchange rate ni bei ya sarafu yetu kama bei za commodities nyingine!!. Mfano mdogo ni hii arguement kuwa kwa kuiachia sarafu yetu iwe rahisi/ yaani shilingi nyingi kwa dollar hivyo exports zetu zinafaidika kwa kupata fedha nyingi; lakini hali halisi ni kwamba toka nchi ianze kupata matatizo ya umeme na mafuta kupanda bei exports zetu zimepungua hence arguement hiyo sio sahihi!! BOT wanatakiwa wawe creative katika kutafuta monetary policy prescriptions ambazo zinaweza kustabilize currency yetu both in the short term na long term!! One suggestion ni jinsi ya kutumia dhahabu tuliyonayo bwerere hapa nchini.
 
Hili nalo ni tatizo kubwa la kitaifa. Tsh inashuka tu kimya kimya.
 
Naona shida hii ya kuanguka Shilling iko kote East Africa. Angalia charts hapa chini:

8D99DNZHLNWdwAAAAASUVORK5CYII=
 
BoT has been printing money to ''save" the TZ economy (they call it quantitative easing) , BUT ........ this is also crushing the TSH
 
Tatizo moja ya watu kama Mdondoaji ni kujaribu kutaka kutatua matatizo yetu kwa kutumia/kuiga jinsi nchi kama marekani inavyotatua matatizo yao ya uchumi na ndio maana wanaquote Ben Barnake anasema nini na kuiga policy prescription zao. Uchumi wa marekani na uchumi wa Tanzania ni tofauti hivyo ni juu ya BOT kutumia njia za kuthibiti mfumuko wa bei relevant to our situation; kwani ikumbukwe kuwa exchange rate ni bei ya sarafu yetu kama bei za commodities nyingine!!. Mfano mdogo ni hii arguement kuwa kwa kuiachia sarafu yetu iwe rahisi/ yaani shilingi nyingi kwa dollar hivyo exports zetu zinafaidika kwa kupata fedha nyingi; lakini hali halisi ni kwamba toka nchi ianze kupata matatizo ya umeme na mafuta kupanda bei exports zetu zimepungua hence arguement hiyo sio sahihi!! BOT wanatakiwa wawe creative katika kutafuta monetary policy prescriptions ambazo zinaweza kustabilize currency yetu both in the short term na long term!! One suggestion ni jinsi ya kutumia dhahabu tuliyonayo bwerere hapa nchini.

Mkuu,

Unanionea bure ndugu yangu narudia tena BOT haiwezi kufanya kitu ndugu yangu tuwe wakweli. Itakachoweza kukifanya ni kuchapisha hela zaidi ziingie kwenye mzunguko ila hilo linaweza kufanya thamani ya shillingi kushuka zaidi. Vile vile kuingiza fedha za kigeni katika soko ni short term solution. Ngoja nikupe solution ya Shillingi nchini kama nilivyowahi kusema kama miezi mingi nyuma tangia march ni hivi:-
a. Wadhibiti dollarisation in the economy matumizi ya foreign currency yamekuwa makubwa mno nchi na hiyo kufanya demand for foreign currencies kuwa kubwa na kushusha thamani ya shillingi nchini.

b. Wakusanye Gold kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo na kutumia gold hizo kuuza nje ya nchi ili kuongeza upatikanaji wa foreign currencies. Vile vile waanze kukusanya gold ili kuipandisha thamani ya shillingi nchini na soko la sarafu nje ya nchi.

c. Wawashinikize makampuni ya madini na makampuni ya mengineyo kuwa listed in local stock market na kuwalipa wafanyakazi wao ni Tshs. Hilo litasaidia kupunguza demand for foreign currencies in Tanzania.

d. Watatue tatizo la umeme nchi ili kuvirudishia uhai viwanda vyetu nchini na kupunguza current account deficit ya nchi.

Ushauri wote huu ni fiscal policy na muhusika mkuu ni wizara ya fedha kwa kushirikiana na hazina. Vyenginezo tunacheza viduku mkuu kwani kuna taarifa dollar itayumba zaidi kuanzia mwezi ujao kwasababu ya mkwaruzano baina ya US na China kuhusu currency exchange. Vile vile madeni ya nchi za ulaya yanaweza kusababisha global recession even possible depression to some countries na hivyo na sie tukaathirika vibaya sana. Tujiandae!!
 
Hatari kubwa sana ya kiuchumi inatusogelea, jioni ya leo baadhi ya maduka ya kubadili fedha za kigeni yalikuwa yananunua dolari kwa Tshs 1,700.

Sijui benki kuu ya Tanzania inachukua hatua gani madhubuti kujaribu kuzuia halii hii?
Hata kama Benki kuu ya Tanzania ikichukua hatua haitosaidia kitu Uchumi wa Nchi umeshuka kwa kiasi kikubwa kila kukicha vitu vinapanda bei.Wanaofaidika ni viongozi wa serikali Mwaziri na Wabunge. Wanaoumia ni akina sisi walala hoi, waache Watu wauze hata dola 1 ikifika sh elfu 2000 poa tu tungojee uchaguzi ujao. Tunataka tupate Serikali inao waonea wananchi wake huruma sio Serikali inaowakandamiza wananchi wake natanguliza hiyo asanteni.
 
tatizo ndio hilo hatuuzi chochote nje kujiongezea akiba ya dola nchini lakini tunanunua kila kitu nje mpaka chumvi,viberiti,nyanya,juice,matunda apple mpaka maji ya kunywa,jamani tunategemea nini?et hadi penseli hatuwezi kutengeneza?kuna viwanda kama vya magunia wawekezaji hawa wahindi wanavigeuza godown badala ya kuzalisha,
Nchi iko gizani karibu mwaka sasa, hakuna tunachouza zaidi ya kugawa kile tulichonacho! Natamani Michael Sata aje Tanzania atusaidie. Pamoja la hayo, sisi tunaowaangalia viongozi wetu wakitusababishia matatizo ni sawa nao tu. Kwani tumebaki kupiga kelele za kichura bila kufanya kile kinachotakiwa.
 
tupunguze matumizi ya mafuta katika magari na mitambo na badala yake tutumie gesi yetu ya songo songo kuendesha magari na mitambo
 
Mkuu,

Majuzi katika mkutano mmoja Ben Benarnke alisema there is little that the Central bank can do to save the country economy. Monetary policy bila ya kuwapo kwa sound fiscal policy ni vigumu sana kuokoa uchumi. Benki kuu itajitahidi kuzuia kuporomoka kwa shillingi kwa njia mbali mbali kama kupunguza pesa za kutoka kwenye mzunguko wa fedha, kuingiza fedha zaidi za kigeni nyingi katika mzunguko nk. But Shida ya monetary policy ni kwamba ni measures za muda mfupi kuokoa uchumi. Serikali inabidi ijitahidi kuokoa uchumi wa nchi kuanguka kwa kutatua tatizo la umeme, ufisadi, dollarisation nk. Bila ya strong fiscal policy BOT itabakia kama bubu kwani ikiingiza pesa zaidi katika mzunguko zitashusha thamani za fedha za kigeni kwa muda mfupi lakini baada ya miezi miwili thamani ya dollar itazidi mara mbili ya ilivyokuwa mwanzo na kuzidisha ugumu wa maisha.

SAFI SANA NI GOOD ECONOMIC ARGUMENT! the matter is how to run economic activities ili kutatua hili swala so f govnt ikilala ndo inakula mdogomdogoka ka msumbiji!
 
Back
Top Bottom