yeye mwenyewe Vasco Da Gama alita shilingi yetu hela ya madafu,sasa kaam hajivunii shilingi yeto u ategemea atakuwa na uchungu nayo,tukubali tu kwamba tuliiingiza chaka kumpa nchi huyu jamaa,kuna watu walisema ati jamaa ni handsome hata kwenye hela akiweka picha yake itapendeza.....mweee!UOTE=Candid Scope;6778817]Pamoja na mapambo ya maelezo kedekede ya wataalamu wa uchumi kutueleza sababu za kushuka au kupanda thamani pesa, kwangu mimi naona kwa Tanzania uzoefu wangu ni tofauti na maelezo yao kabisa.
Kipindi cha uongozi wa Nyerere tulishuhudia pesa kushuka thamani kwa kiwango kidogo mno, na sababu kubwa Nyerere hakuwa na hulka ya kujenga uchumi tegemezi wa kuombaomba huku na kule. Alitumia rasilimali na mapato ya humu humu nchini, ingawa kulikuwa na miradi kadhaa ya maendeleo iliyofadhiliwa hasa na nchi za China na Japan, hata hivyo ilikuwa ni kwa kiwango kidogo.
Kipindi cha Mzee Ruksa mfumuko wa bei ulianza kuinuka zaidi na inaeleweka kwa sababu ya sera za mfumo wa uchumi wa biashara huria na utandawazi alipofungua mapazia kuruhusu hewa mpya iingine na watu kuanza kujigonga vichwa vyao kwenye vioo kushangaa vitu vinavyozidi kumiminika madukani. Hata hivyo deni lilionekana kuongezeka kipindi Cha Mzee Ruksa sababu siwezi kujua kwa ndani maana muda huo mambo ya serikali yalikuwa ya siri kali huko Mkulu na baraza lake la mawazini, na Mrema alipotaka kuhoji basi alipata kichapo na kusukumiwa nje ya uringo kwa sababu alikuwa anarusha ngumi isivyokubaliwa na mwamuzi wa pambano.
Nzee Nkapa alipoingia madarakani, alishtushwa na deni kubwa la Taifa na hivyo kufanya diplomasia na mataifa yale yanayotudai kushawishi yatupe unafuu kwa kufuta, na alifanikiwa mataifa mengi yalifanya hivyo. Nzee Nkapa akaanza namna yake ya kujenga uchumi wa kujitegemea kwa kuanza miradi ambayo chanzo cha mapato kilikuwa hapa hapa nyumbani kama bomba la maji toka ziwa Viktoria, na ujenzi wa Daraja kwenye mto ruvuma kuunganisha Msumbiji na Tanzania.
Alipoingia Vasco da Gama akaFaster Jet ni kama mtu mwenye mapepo vile, maana pale Ikulu hapakaliki sijui kuna mapepo yanamsukumia nje? Ni kurukaruka huku na kule kutembeza bakuli hata yule hayati ombaomba wa Dodoma hafui dafu. Obama amemwonya kiaina aliposema Afrika itajengwa na waafrika wenyewe, lakini sijui Kama Faster Jet alimwelewa, alibaki kuchekacheka tu na kuwashangaa wazungu walioongozana na Obama kana kwamba hakuwahi kuwaona na kuwavutia wamtazame usoni anapochekacheka.
Uchumi 75% tegemezi tautazamie nini?
Deni la taifa limepaa isivyo kawaida tangu nchi hii ipate uhuru haijatokea. Deni hilo ni kutokana na kupitisha bakuli huku na huko kila kukicha na anachokinga kwenye bakuli hatukioni huku akitumia mabililioni kuruka huku na huko na anachoambalia aendako hakijai kwenye kiganja huku akiwavutia kuja kusomba rasilimali za taifa letu ambazo ndizo zingetumika ilivyo ndizo zingepandisha dau la thamani ya pesa yetu.
Thamani ya Pesa itazidi kuporomoja tu kwa mtindo wa kutegemea maisha ya kuombaomba tofauti na nchi ambazo zimesimama kwa uchumi wa kujitegemea.
[/QUOTE]