Shilingi 7,000 kwa siku utaishi vipi?

Shilingi 7,000 kwa siku utaishi vipi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,713
Reaction score
57,235
Hi kwa mfano unafanya kazi kwenye kiwanda kipo Mbagala na kinakulipa 7,000 kwa siku utaishi vipi endapo nauli unatumia 1000,chakula 3000,vocha na maji 1000. Hapo bado hujalipa kodi ya chumba na mahitaji mengine ya familia. Tuweni serious jamani 10,000 sio hela kwa siku inaisha haraka sana sasa sijui nini maana ya viwanda kama ujira wenyewe ndo mdogo kiasi hicho?
 
hivi kwa mfano unafanya kazi kwenye kiwanda kipo mbagala na kinakulipa 7000 kwa siku utaishi vipi endapo nauli unatumia 1000,chakula 3000,vocha na maji 1000.hapo bado hujalipa kodi ya chumba na mahitaji mengine ya familia.tuweni serious jamani 10000 sio hela kwa siku inaisha haraka sana sasa sijui nini maana ya viwanda kama ujira wenyewe ndo mdogo kiasi hicho?
Kupanda gari ni starehe si utembee kwa mguu? Mbona babu zetu walikuwa wanatoka tbr to dar through slave trade?
 
hivi kwa mfano unafanya kazi kwenye kiwanda kipo mbagala na kinakulipa 7000 kwa siku utaishi vipi endapo nauli unatumia 1000,chakula 3000,vocha na maji 1000.hapo bado hujalipa kodi ya chumba na mahitaji mengine ya familia.tuweni serious jamani 10000 sio hela kwa siku inaisha haraka sana sasa sijui nini maana ya viwanda kama ujira wenyewe ndo mdogo kiasi hicho?
hauishi hapo ni kunywa sumu tu na kufa
 
Vocha kila siku?
Nauli kila siku kwenda na kurudi?
Mara moja moja jioni weka utaratibu wa kurudi nyumbani kwa kutembea. Asubuhi nenda kwa gari ili uokoe muda, kama si mbali sana amka mapema chapa raba.
 
Wizi,rushwa,kujipendeza,utapeli unaanziaga huku nashauri serikali ianzie kwenye kuboresha maslahi ya wafanyakazi ndipo waanzishe vita ya rushwa
 
Kama unalipwa hela hiyo kwa nini ukae mbali na sehemu ya kazi? Tafuta makazi nafuu yaliyo jirani na hicho kiwanda na kisha tafuta utaratibu utakaokupunguzia gharama za Maisha kama chakula, maji na mengineyo. Otherwise tafuta shughuli itakayokuingizia kipato Zaidi au fanya kazi Zaidi ya moja
 
Kwani vijana wa Lumumba wanaishi vipi??

On a serious note..7k ni kidogo,ila kuna watu wana hali ngumu kiasi kwamba hii hela wakiipata inakuwa mwokozi wao..
 
Mkuu nbagala kuna supu hadi ya tsh 200,hadi umalize 7000tsh utakuwa ni utakatishaji wa pesa
hivi kwa mfano unafanya kazi kwenye kiwanda kipo mbagala na kinakulipa 7000 kwa siku utaishi vipi endapo nauli unatumia 1000,chakula 3000,vocha na maji 1000.hapo bado hujalipa kodi ya chumba na mahitaji mengine ya familia.tuweni serious jamani 10000 sio hela kwa siku inaisha haraka sana sasa sijui nini maana ya viwanda kama ujira wenyewe ndo mdogo kiasi hicho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom