Tundu Lissu mmojawapo wa wagombea uchaguzi Mkuu 2020 ambaye anazunguka kuomba ridhaa. Watanzania tuna kila sababu ya kumuhoji Lissu maswali haya.
Lisu huyu ndiye yule aliyekuwa akiwatetea ACACIA kwenye suala la madini, kwanini aungane na waliokuwa wanaiibia nchi na kuanza kuwatetea? Akaenda mbali akawa anatutisha Watanzania kuwa tutashtakiwa wakati akijua wazi hatuwezi kushtakiwa, alikuwa akiyafanya haya kwa faida ya Watanzania kweli?
Wengine watasema ni haki yake, sawa ni haki yake tufanye. Ni haki sahihi kuwatetea wezi wa madini yetu? Ni haki kubariki kuibiwa na kuachiwa maandaki na umaskini na wanyonyaji wa rasilimali hizi?
Jambo jema yule aliyekuwa akiwatetea wezi wa madini yetu ndio huyo huyo anaomba ridhaa wakati ambao Dunia itashuhudia Oktoba 13, 2020 kampuni ya Barrick Gold ikitoa fidia ya gawio la zaidi ya Tsh. Bilioni 100 ambayo ni matunda ya mikataba ya madini na sheria zinazolinda maliasili na madini ya Tanzania.
Watanzania muulizeni Lissu mbona hatujashtakiwa kama alivyosema? Mbona aliosema wana haki ndio wanaotupa gawio la Mabilioni ya fedha?
Ni Lissu huyu huyu pasi na haya alishiriki kuhujumu ndege zetu ili zikamatwe, kwanini aliamua kuhujumu mali za Taifa? Ni kwa faida ya Watanzania ama faida ya Mabeberu anaowatumikia? Anaendaje kuomba kura kwa Watanzania aliowasaliti?
Lissu aendelee kutueleza nini maana yake kuwasimanga, kuwananga, kuwadhihaki Watanzania kuwa ni maskini wakati huo anawaomba michango ya kampeni! Mtu maskini na mwenye uchumi mbovu utamwombaje michango? Atatembezaje bakuli kwa Watu maskini?
Ni Lissu huyu huyu anaomba kupigiwa kura wakati yeye mwenyewe hajajiandikisha na hajaboresha taarifa zake kwenye daftari la Wapiga kura! Watanzania wampigie kura asiyeweza kujipigia kura?
Shilatu, E.J