Tisha-TOTO
JF-Expert Member
- Feb 10, 2010
- 1,175
- 604
Shikamooni Wakuu,
Jina langu si hoja. Adabu iko palepale kwenu wakulu...
Shalom!
Jina langu si hoja. Adabu iko palepale kwenu wakulu...
Shalom!
Shikamoo salamu za kitumwa wengine hatuzi mind kabisa hizo.
Shikamoo ni chakula ya babako sisi hakitufai!!Shikamooni Wakuu,
Jina langu si hoja. Adabu iko palepale kwenu wakulu...
Shalom!
Kiranga na wewe .....hahaaaaaa nicheke tu mie?? maana yake nini kwanza 'shikamoo'?
Maana yake "nakushika miguu yako" au "niko chini ya miguu yako". Ni salamu iliyoanza kutumika katika enzi ya utumwa, watwana na watumwa wakiwaamkua mabwana zao, yaonyesha nani mtwana/mtumwa na nani bwana.
Ndiyo maana kuna wazee wengine wanaoielewa maana yake ukiwaambia hawasemi "marhaba" wanasema "ahsante" au wengine wanakataza kabisa kuamkiwa shikamoo.
Kama unaelewa historia ya biashara ya utumwa, na unaelewa historia ya shikamoo, na una utu wa ku sympathize na weusi walivyoteswa, huwezi kukubali shikamoo.
Niwie radhi kama nimekukosea mkuu na wakuu wengine wote. Kupotea njia ndio kuijua. Naomba mnielimishe kidogo namna gani iliyo bora ya kuonyesha heshima unapowaamkia unaowaheshimu?Shikamoo ni chakula ya babako sisi hakitufai!!
Wakuu mimi Mfipa, kutokea Sumbawanga,
Sijavibeba vichupa, hivyo mimi siyo mwanga,
Tabanana hapahapa, Dar pande za Keko Mwanga,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!
Kwa kweli ushamba umo, naomba kuvumiliwa,
Nasabahi kwa shikamoo, kumbe hili kosa kubwa!
Nahitaji pata somo, kutoka kwenu wakubwa,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!
JF ni bahari, iliyojaa hazina,
Najisikia fahari, kuwakuta waungwana,
Ninawatakia heri, ya mwaka mpya mwanana,
Msinicheke ushamba, ila mnipige shule!!
Wee ni mfipa kweli? Mbona una mashairi ya kimwambao? Au ndio ile pwani ya Lake Rukwa??!Wakuu mimi Mfipa, kutokea Sumbawanga,