SHIKAMOONI wachoma nyama pale mikumi mbugani

SHIKAMOONI wachoma nyama pale mikumi mbugani

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
419
Napenda kuwapa tano wachoma nyama ya mishikaki na ndizi pale mikumi ukitokea Morogoro, kwa kweli nyama zenu ni tamu hatari na kubwa si mchezo mpaka raha, nikipitaga mikumi lazima ninunue mishikaki kama rambo 2 hivi, ni kutafuna kwa kwenda mbele mpaka Iringa, ila isije kuwa mnatulisha nyama za mbwa na paka, eti mnalipaga TRA kwa kuuza hizo nyama? Shauri zenu Magufuli anakuja
 
maeneo yangu hayo !!ila huwa najiuliza kama ni ngombe kweli!!

umeona mkuu ki ukweli nyama zao na ndizi ni bomba sana ila swali ni za ngombe kweli? isijekua wanatulisha madudu mbwa.
 
Ama kweli wanastahili pongezi hususa wale wamasai wanaochoma nyama ya mbuzi. Pale huwa nachukua mguu mzima wa mbuzi.
 
napenda kuwapa tano wachoma nyama ya mishikaki na ndizi pale mikumi ukitokea morogoro, kwa kweli nyama zenu ni tamu hatari na kubwa si mchezo mpaka raha, nipitaga mikumi lazima ninunue mishikaki kama rambo 2 hv, nikutafuna kwa kwenda mbele mpaka iringa, ila isije kuwa mnatulisha nyama za mbwa na paka, eti mnalipaga TRA kwa kuuza hizo nyama? shauri zenu magufuli anakuja

Mkuu siku ukienda Kampala ukivuka Masaka usisahau kupita hapo
 
Ila pale sio mikumi ila toka pale kuna mwendo kidogo kufika mikumi, ni mbele kidogo toka njia panda ya kwenda Mzumbe, jina lake nimesahau kidogo. Mishikaki ya pale mingi ni ya mbuzi, kwa kweli ni mitamu sana.
 
Wanauza shillingi ngapi na sisi tukipita tununue?
 
Ni maeneo ya Mkata, nimepita hapo kwenye saa Nne asubuhi leo, naelekea Kyela.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom