Shikamoo mapenzi

Shikamoo mapenzi

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
LAITI kama maumivu ya mapenzi yangekuwa yanaacha alama kabisa ..yaani kama umeumizwa linatokea NUNDU, ama JINO LINANG’OKA, au kama ni MCHUBUKO USONI, ama ukiyaendekeza sana YANAKUTEGUA MGUU, MKONO, ukizidisha zaidi YANAKUTENGUA KIUNO….

#Nadhani ni MACHANGUDOA peke yao wangekuwa warembo Duniani..……na wanafunzi wa vyuo vikuu wasichana wangeongoza kwa kuwa wanawake wenye SURA MBAYAAAA.......wanatendwa haooooo.......

NA hii ingesaidia sana watu kujiepusha na mapenzi hovyo hovyo maana unakuta mtu analalamika oooh mapenzi yanaumiza. Kesho keshokutwa ana mpenzi mpya, hajakaa sawa oooh mimi na mapenzi basi nimeumizwa sana, baada ya wiki moja anaaga kuwa anaenda kwa mpenzi wake mpya…….mapenzi kama yanakuumiza pumzika ndugu..we hujipi likizo unakaa kulia lia tu hapa naumizwa naumizwa….
Mi nadhani nyie mnaolialia kila siku kuwa mnaumizwa tuwaunganishe kwa pamoja mtunge wimbo naamini utakuwa wimbo mzuri sana maana dah….mnanifurahishaga na malalamiko yenu kama vile kawimbo ukigusa tu..'Mi naogopa nilishaumizwa...mimi sitaki tena utaniumiza'
Ndo maana nasema hivi yangekuwa yanaumiza kisawasawa yaani yanakubutua kama lingumi hivi usoni weeeee mbona yangeheshimiwa….tatizo hatuyaheshimu mapenzi ndo maana na yenyewe yanatudharau…..
Mfano mtu akiona mwenzake kapata ajali ya bodaboda mbona anaapa kuwa hapandi tena…..

SASA iwe hivyo na kwenye mapenzi ukiona mwenzako kavunjwa kiuno na meno yamebaki mawili mdomoni utashika adabu yako na mapenzi…..
Ukienda kichwa kichwa yanakutandika bonge la kofi usoni mbona akili itasogeleana……
Maumivu ambayo hayaonekani si hata muigizaji anaweza kujidai kaumizwa…wewe yakuchane kabisa uso mbona utasema ‘Poo’

@# sijui hata nawaza nini ….lakini SHKAMOO MAPENZI….
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom