Shida yangu na NHIF ni pale kadi inapoandikwa ile tarehe uliyolipia kama tarehe ya kuanza matumizi badala ya ile tarehe uliyoambiwa uchukue kadi

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
494
674
Umekuwa ni utaratibu wa kawaida kabisa unapokata bima ya afya kutakiwa kusubiri miezi 3. Hili mimi sina shida nalo. Shida yangu ni pale kadi inapoandikwa ile tarehe uliyolipia kama tarehe ya kuanza matumizi badala ya ile tarehe uliyoambiwa uchukue kadi. Mfano.

Unapolipia kadi december unatakiwa ukachukue kadi march. Hii ina maana unalipia mwaka ila kadi ina uhai wa miezi 9. Bado unaenda baada ya miezi 3 unaambiwa bado.

Hivyo uhai wa kadi yako umazidi kupungua. Kuna watu wanalipia kadi kwa mwaka ila mpaka waipate kadi miezi 4 omeshaisha
Haki hapa iko wapi?

Sio wizi huo?

Kwanini tarehe ya kuanza kutumika isiwe ile tarehe ya kuichukua?

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom