KERO Shida ya maji Ruangwa imezidi sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Tujiandae tukatiki Oktoba 29 shida ya maji itakuwa historia๐Ÿฅณ
 
Pole sana,hamia pale kijiji cha Nandagala kuna ukuta mkubwa juu ya kilima mule maji 24/7 kwa nini uteseke.
 
Hapo bora wangeprint bango moja kubwa.
Mabango makubwa yapo tayari. Huku kuna kila size ya bango, nyumba za watu masikini wamebandika kazi na utu kwenye milango na kuta za nyumba zao za udongo. Taa za barabarani, majengo ya watu kila kona kuna mabango ya kutosha ya size tofauti tofauti

Kama ni kura huku wameshapata. Mi sijali walete tu maji
 
Kwa ruangwa mjini kilichobaki maji na flyover bc๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Aweso na CCM yote wamefeli kwenye issue ya maji japo wanajisifu eti wamemtua mwanamke ndoo kichwani. Labda wanamaanisha wamemtwika. Hilo ni tatizo kwenye miji yote ya hii nchi ya Samia. Kwenye kila mji, huwa kunakuwepo ka kikundi kadogo ka wakazi (wakiwemo viongozi wa serikali na vigogo wengine) ambao wanapata maji muda wote. Halafu wanatumia takwimu za hao wachache kutudanganya kuwa hakuna shida ya maji.
 
Kwa ruangwa mjini kilichobaki maji na flyover bc๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Ni kweli sisi maji ndo yanatuharibia, maana haka ni kamji kadogo ila hakana changamoto nyingi
Umeme haukatiki sana, shule hazikuwepo sasahivi zimejaa tele, barabara kila mtaa wameweka lami na taa za barabarani, na bado wanaendelea kujenga barabara. Kuna uwanja wa mpira, wamejenga hospitali nzuri, Internet mitandao yote inashika 4G vizuri sana, watu wanaongezeka na sasahivi nimeanza kuona kidogo watu wameanza kujenga nyumba nzuri

Wanajenga lami kwenda moja kwa moja hadi Nachingwe sasahivi. Inatoka Nachingwea hadi hapa Ruangwa na inaendelea hadi kwenda njia ya Mbekenyera. Hii barabara inaendelea na ujenzi niliipiga picha juzi
 
Advance nimesoma Mbeya, kule hakukuwa na shida ya maji
Ila maeneo mengi ya Tanzania maji ni shida. Sasa kwa nini wanatudanganya kuwa hakuna shida ya maji. Unajua huwezi kusolve tatizo kama ukijidanganya eti hilo tatizo halipo
 
Katikati ya michenga na chimbila a pana tank kubwa mno je halijaanza kazi?
 
Pole sana Luca Paguro, Ila wewe ni snitch ulimkataa mwanao baada ya kubadilika kwenye maji kisa demu, ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Kijana kuwa na subira, Kuna miradi mkubwa wa maji ya kutoka chanzo Cha Nyangao, mradi huu ukikร milika utahudumia kata za njiani za Malolo, Nandagala,Mnacho, Chienjele, Nkowe , Likunja na kata zote za mjini(kata za Ruangwa na Nachingwea), na vijiji baadhi vya wilaya ya Nachingwea mfano baadhi ya vijiji vya kata ya Chiola(Mtimbo, Chiola A na B, Namauni na Chingunduli).
Kwa Sasa mradi upo katika hatua ya kuunganisha mabomba ya line kuu, Kwa upande wa ujenzi wa matanki tayari umekamilika. Kata ya Malolo Tanki limejengwa kati ya Kijiji Cha Michenga na Chimbila A, pia Kuna Tanki lingine limejengwa juu milimani katika Kijiji Cha Chimbila A, Tanki lingine katika Kijiji Cha Nandagala
 
Pole sana Luca Paguro, Ila wewe ni snitch ulimkataa mwanao baada ya kubadilika kwenye maji kisa demu, ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
Alberto alizingua mwenyewe alikuwa na wivu wa kijinga, pale bila kumsnitch maana yake Giulia angejua na mimi ni sea monster ๐Ÿ˜…
 
Barabara hii ni nachingwea to kilanjelanje mkeka tupu hiyo ukifika nanjilinji pale mto mbwemkulu wachina wanakesha wanajenga daraja kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ