KERO Shida ya maji Ruangwa imezidi sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Luca Paguro

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
499
Reaction score
1,125
Ruangwa tuna shida kubwa ya maji. Mimi nimezaliwa hapa nimekulia hapa hadi leo hii nakaribia umri wa miaka 20 miaka yote hapa tuna shida ya maji tu, tangu niko mdogo tunateseka na shida ya maji hadi leo hii bado tunaendelea kuteseka. Nothing is getting better

Huku maji yanatoka mara moja kwa wiki, yakijitahidi sana mara mbili. Na kutoka kwake yanatoka kwa saa 1 tu halafu yanakata. Kwa wiki nzuri tukibahatika maji yanatoka kwa masaa mawili.

Maana yake hata tank halijai, maji ya tank yanaisha mnabaki hamna maji. Siku nyingine yanatoka maji machafu bombani yanakuwa na rangi nyekundu kana kwamba yamechanganyika na udongo, siku nyingine pia yanatoka kwa spidi ndogo mno hata kwenye tank hayapandi

Maji yenyewe ya chumvi halafu wanabania, yanatoka saa 1 kwa wiki. Bila kisima hutoboi

Nyinyi watu mnaohusika na usambazaji wa maji Ruangwa, leteni maji hata mara tatu kwa wiki, kila siku yatoke masaa mawili mawili basi tupate walau masaa 6 kwa wiki. Maana tunateseka sana wakazi wa haka kamji
 
Ndio kwa Katelefon huko?
Ndio huku, wametuletea barabara za lami kibao, street lights kibao, uwanja wa mpira, shule za kutosha, halafu wakasahau kutuletea maji
Bora hata wangetupa maji kwanza kabla ya hivyo vitu vingine. Yani wanabania kinoma halafu maji yenyewe ya chumvi. Watu wake wamezoea kuvumilia hii shida

Huku wameweka lami nyingi na watu hata magari hawana. Wangeanza na MAJI kwanza, maana lami za mtaani hata hazina ulazima kihivyo
 
Huko si kulikuwa kwa top 3 au
 
Mwaka 2020 kuna jamaa aliwachimbia visima huko kwenu, Katelefon akapewa taarifa kuwa jimboni kuna mvamizi, kilitokea nini kwa yule jamaa?
 
Sorry hata hiyo saa moja kwa week inabidi ushukuru kijana. ila 29/10 Ukitiki tutafanya yatoke saa moja na nusu. Ccm oyee
 
Mbona kwenye mikutano tunasikia mkisema "mama hatukudai kitu"
Tatizo ni elimu mkuu. Huku watu wengi hawajaelimika. Wao akija kiongozi ni kumshukuru tu hadi wanagalagala chini. Sasa kwa hali hii hata viongozi hawatajua shida tulizonazo
 
Mwaka 2020 kuna jamaa aliwachimbia visima huko kwenu, Katelefon akapewa taarifa kuwa jimboni kuna mvamizi, kilitokea nini kwa yule jamaa?
Tusaidie kujua
 
Mwaka 2020 kuna jamaa aliwachimbia visima huko kwenu, Katelefon akapewa taarifa kuwhuua jimboni kuna mvamizi, kilitokea nini kwa yule jamaa?
Huu ni uongo hivyo visima vilichimbwa wapi kwanza tuanzie hapo?
 
Hii ni kweli hata kasimu mwenywe halifichagi jambo hili kuhusu uhaba wa maji ila mwamba alijitahid kuyavuta maji kutoka nyangao kuja ruangwa ukifika michenga pale Kuna tanki kubwa limejengwa kwa ajili ya mradi huo sasa cjuw na HIV anavyostaafu kama hawataubadili mradi ukawa mfu tuombe mungu
 
Duh... Kama wameshaanza mradi basi waumalizie tu, maji yatufikie. Viongozi wasije wakala pesa za mradi halafu sisi tukaendelea kuteseka tu, hali si shwari kabisa.
Maana mimi Ruangwa mjini sioni changamoto nyingine tofauti na maji. Walete maji jamani, hizi pesa za huu mradi mafisadi waziache tu, chonde chonde 😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…