Shida ya maji mbezi high school mpaka mpigi magoe

Jewel

Senior Member
May 1, 2008
176
62
Mbezi high mpaka Mpigi Magoe kuna tank maeneo hayo kuna mradi wa maji uliokamilika lakini haujazinduliwa rasmi ni.. hivi karibun tumekua tukipata maji vizuri lakin kuanzia wiki iliyo pita hatuna maji, hakuna ufafanuzi wa kina unaotolewa zaid ya kua tu kuna changamoto ila hakuna dalili yoyote ya mafundi kuona kuwa wana shughulikia tatizo hilo, tunapata tabu sana, tuna omba tatizo hili lishighulikiwe mara moja.Ajabu magari ya maji yameanza kutembea kwa kasi na kuuza maji mitaani .Tunakuomba Mheshimiwa Rais uliangalie hili kwa jicho la karibu .
 
Kumbushia ile barabara ya mbezi - mpigi magoe iwekwe lami kwanza. Haya mambo ya kuweka kifusi kila baada ya miezi kadhaa siyo sustainable
 
Katika vitu serikali inabidi itoe kipaumbele ni barabara ya mpiji magoe kuanzia pale stand ya magufuli mpaka bunju B ipigwe lami

Wakazi wa mpiji magoe wanateseka sana kutokana na usafiri kuwa wa shida kutokana na ubovu wa barabara

Daladala zilishagoma, hata gari za mikoani zinazoensa kaskazini kupitia bagamoyo hii ndo njia rahisi zaidi kuliko kuzunguka mpaka kule madale
 
Kifusi wameweka lini? Toka Rais Magufuli afe ile barabara imekuwa kama sehemu ya watu kupigia hela.
Zamani ilikuwa haipiti miezi mitatu ishachongwa, lakini siku hizi imejaa mashimo hakuna kiongozi wala wahusika(TANROADS DSM) anayejali. Mbunge kapeleka lami kwake Kibamba na wala hatujui sikuhizi yupo wapi, wananchi wamebaki kulalamika tu, hakuna cha mkuu wa wilaya wala Mbunge anajali.
 
Mkuu unaweza kupiga picha ya mashimo kwenye barabara hiyo
 
Katika vitu serikali inabidi itoe kipaumbele ni barabara ya mpiji magoe kuanzia pale stand ya magufuli mpaka bunju B ipigwe lami

Wakazi wa mpiji magoe wanateseka sana kutokana na usafiri kuwa wa shida kutokana na ubovu wa barabara

Daladala zilishagoma, hata gari za mikoani zinazoensa kaskazini kupitia bagamoyo hii ndo njia rahisi zaidi kuliko kuzunguka mpaka kule madale
Wakazi wa huko mtakuwa mnapata tabu sana. Lakini mama ni msikivu sidhani kama ataacha watu wateseke hivyo. Lazima atafanya jambo kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Natumaini hiyo Barbara imetengewa hela na bunge
 
Barabara ya Mpigi magohe ni kero kwa Wananchi wote wa huku,Nitapiga picha kisha mtuambie mnampango gani na hii barabara.Sidhani kama kuna mtu ataipitisha CCM kwa hizi huduma za jamiii huku.
 
Mbezi high mpaka Mpigi Magoe kuna tank maeneo hayo kuna mradi wa maji uliokamilika lakini haujazinduliwa rasmi ni.. hivi karibun tumekua tukipata maji vizuri lakin kuanzia wiki iliyo pita hatuna maji, hakuna ufafanuzi wa kina unaotolewa zaid ya kua tu kuna changamoto ila hakuna dalili yoyote ya mafundi kuona kuwa wana shughulikia tatizo hilo, tunapata tabu sana, tuna omba tatizo hili lishighulikiwe mara moja.Ajabu magari ya maji yameanza kutembea kwa kasi na kuuza maji mitaani .Tunakuomba Mheshimiwa Rais uliangalie hili kwa jicho la karibu .
Sio huko tu Babu ni Dar nzima hakuna maji ukame tu maji yanatoka usiku wanafunguliwa vibopa fulani watu wakiwa wamelala wajaze matank yao asubuhi hukuti maji mchana hukuti maji usiku amka saa 8 maji yapo ikifika saa 12 asubuhi wanapiga lock nimekutobolea Siri
 
Wakazi wa huko mtakuwa mnapata tabu sana. Lakini mama ni msikivu sidhani kama ataacha watu wateseke hivyo. Lazima atafanya jambo kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Natumaini hiyo Barbara imetengewa hela na bunge
Sitaki kugusagusa haya masuala hawachelewi kukupiga ban hawa watu, ukigusa tu masuala ya barabara jiangalie mara 2 JF utaisikie ukiwa nje ban itakutembelea very soon
 
Kumbushia ile barabara ya mbezi - mpigi magoe iwekwe lami kwanza. Haya mambo ya kuweka kifusi kila baada ya miezi kadhaa siyo sustainable
Achana na masuala ya barabara utachezea ban usiseme sikukwambia shauri yako,
 
Swala la maji Dar ni km enzi za before Magu mjini joto and no water or power plus mfumuko wa bei hali nimbaya sn tena mno,halafu 2025 mnasema mama tena kura yangu imepotea tyr kwakweli
 
Back
Top Bottom