Misuli ya macho kutetemeka/twitching, inaweza kuwa si dalili ya ugonjwa au tatizo lolote kubwa la kiafya.
Hii huweza kutokana na kuchoka, kukosa usingizi, matumizi ya kahawa, stress au kuwa kwenye kazi ya kuangalia screen/sklini kwa muda mrefu mfano: komputer, simu, Tv nk.
Suluhisho: kupunguza au kuondoa hayo hapo juu. Mfano: Pata muda wa kupumzika, punguza au jifunze kuishi na stress, punguza matumizi ya kahawa au punguza matumizi ya sklini.
Baada ya siku au wiki tatizo litaondoka.
Kama pamoja hayo tatizo lisipoondoka basi waone wataalamu wa afya.