FT: Ufaransa 3-1 Senegal | World Cup 2026 | MetLife Stadium | 16 Juni, 2026

FT: Ufaransa 3-1 Senegal | World Cup 2026 | MetLife Stadium | 16 Juni, 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,865
Reaction score
6,364
Timu ya Taifa ya Senegal imekubali kichapo hicho katika Kundi I, licha ya kuanza kucheza vizuri kipindi cha kwanza cha mchezo huo, kipindi cha pili mbinu za Ufaransa zikawa bora na kupata magoli kupitia kwa Kylian Mbappe dakika ya 66 na 90 na Bradley Barcola (82).

Senegal imepata goli lake kupitia kwa Ibrahim Mbaye (90). Michezo ijayo kwa timu hizo; Ufaransa itaivaa Iraq, Senegal ikikipiga dhidi ya Norway, michezo yote ikitarajiwa kuchezwa Juni 22, 2026.
HK9mnziXwAEiLW6.jpg

HK9mnztXoAAeCMP.jpg
====================


Kiuhalisia hawa wote ni Waafrika tu, maana Ufaransa ina wachezaji wengi wenye asili ya Afrika. Hii ni moja ya mechi tamu zaidi kwenye World Cup 2026. Sasa sijui niwe upande gani, maana timu zote mbili nazishabikia.
  • Ufaransa: Kama Deschamps akifikisha timu hii mbali, ataweka jina lake kwenye vitabu vya historia kwa kuwa rekodi ya mechi nyingi zaidi kuongozwa na kocha mmoja ni mechi 25. Baada ya kufika fainali mbili zilizopita mfululizo, Ufaransa inalenga kuwa timu ya tatu tu katika historia kufika fainali tatu za Kombe la Dunia mfululizo. Walifuzu kwa rekodi nzuri (Ushindi 5, Sare 1), na wameshinda mechi 9 kati ya 11 zilizopita (Sare 1, Fungwa 1).
  • Senegal: Walifuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa hawajapoteza mechi hata moja (Ushindi 7, Sare 3). Hata hivyo, katika mashindano yaliyopita hawajawahi kuvuka hatua ya 16 bora tangu walipofika robo fainali mwaka 2002. Changamoto kubwa kwa Senegal ni kwamba hawajaruhusu lango lao kuwa salama (clean sheet) katika mechi 11 zilizopita za Kombe la Dunia, na hawakushinda mchezo wowote wa kirafiki wa kujiandaa na mashindano haya (Sare 1, Fungwa 1).

Historia ya Timu Hizi (Head-to-Head)​

  • Kumbukumbu ya Mwaka 2002: Mara ya mwisho na ya pekee timu hizi kukutana ilikuwa mwaka 2002, ambapo Senegal iliishangaza dunia kwa kuifunga Ufaransa goli 1-0 katika mchezo wa ufunguzi.
  • Mwiba wa Timu za Afrika: Ufaransa imekuwa na wakati mgumu dhidi ya timu kutoka Afrika hivi karibuni, ikipoteza mechi tatu kati ya nne zilizopita za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia zilizochezwa dhidi ya timu za bara la Afrika.
Soma Pia: 2026 FIFA World Cup - Special Thread

Updates


Hadi sasa dakika 8 Senegal wanamiliki mpira kwa asilimia 55 dhidi ya Ufaransa
 
Sisi wahenga Hii mechi inatukumbusha kipira kilichopigwa katika jiji la SEOUL South Korea, siku ya Ijumaa may 31 2002.
Kwa ukanda wetu ilikuwa mapema asubuhi, wakati Senegal wameishangaza Dunia dhidi ya bingwa mtetezi Ufaransa akiwa na kikosi chake hatari kabisa.
Majina yasiyojulikana yalisimama kulinda heshima ya nchi yao na bara zima la Afrika.
Bado tunawakumbuka baadhi yao.

Papa Bouba Diop 'rip'
Khailou Fadiga
Al Haji Diof
Souleman Camara
Ferdinand Koly
Habib Beye na wengine
 
Sisi wahenga Hii mechi inatukumbusha kipira kilichopigwa katika jiji la SEOUL South Korea, siku ya Ijumaa may 31 2002.
Kwa ukanda wetu ilikuwa mapema asubuhi, wakati Senegal wameishangaza Dunia dhidi ya bingwa mtetezi Ufaransa akiwa na kikosi chake hatari kabisa.
Majina yasiyojulikana yalisimama dhidi ya nchi yao na bara zima la Afrika.
Bado tunawakumbuka baadhi yao.

Papa Bouba Diop 'rip'
Khailou Fadika
Al Haj Diof
Souleman Camara
Ferdinand Koly
Habib Beye na wengine
Cisse,Camara,Papa Bouba Diop ,Al Haj Diof na kocha Bruno Metsu
 
Pia kongole ziende kwa kipa wa verde bila zile save za maana spain wangeondoka na ushindi jana, spain walipiga mpira mwingi basi tu haikuwa siku yao
Verde sio wabaya ila ukiwaweka kwenye mizani, Spain ipo mbali. Kile kikosi kilivyotoka cha Spain nikawa naiona kabisa draw hii hapa.
 
Sisi wahenga Hii mechi inatukumbusha kipira kilichopigwa katika jiji la SEOUL South Korea, siku ya Ijumaa may 31 2002.
Kwa ukanda wetu ilikuwa mapema asubuhi, wakati Senegal wameishangaza Dunia dhidi ya bingwa mtetezi Ufaransa akiwa na kikosi chake hatari kabisa.
Majina yasiyojulikana yalisimama dhidi ya nchi yao na bara zima la Afrika.
Bado tunawakumbuka baadhi yao.

Papa Bouba Diop 'rip'
Khailou Fadika
Al Haj Diof
Souleman Camara
Ferdinand Koly
Habib Beye na wengine
Umenikumbusha mbali sana,

Diop alifunga goli la kwanza la mashindano Ya WC 2002 opening match,alimaliza mpira uliopigwa na El Hdji Diouf baada ya kuzuiwa na Barthez,

Senegal vs France,goli likadumu mpaka mwisho wa mchezo,

Chini ya kocha Bruno Metsu R.I.P
 
Back
Top Bottom