Shida sugu ya maji Korogwe, Tanga

Shida sugu ya maji Korogwe, Tanga

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Wakuu.

Mji wa Korogwe ambao upo Wilaya ya Tanga ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi sana na ni Mji kiungo kibiashara kati ya Lushoto, Tanga, Dsm, Moshi /Arusha, Morogoro.

Ni Mji ambao unapitiwa na barabara kuu na reli ambayo miundombinu yake imekarabatiwa vizuri.

Mji wa Korogwe unapitiwa na mto mkubwa wa Pangani unapita katikati.

Kuna mito mingine ya kudumu kama Soni, Mkomazi, Lwengera, Nkole, Vumuni n.k

Shida ya maji Korogwe Mjini ni ya muda mrefu sanaaaa, maji ya kunywa hakuna kabisa.

Kwa mwezi maji yanatoka mara mbili mpaka 3 kwa mwezi mzima.

Shida ni nini ? Wataalamu wa Maji au viongozi wa serikali au Siasa Wilaya ya Korogwe?

Mito ipo yenye maji mwaka mzima.
 
Wewe ulioko huko Korogwe hujui tatizo, unategemea sisi tulioko Iringa tukujibu Nini?

Hapo Korogwe najua hakuna DED Ila DC yupo, mbunge aliye oa juzi juzi yupo, DAS yupo na madiwani wapo hata engineer wa maji yupo.
 
Hakuna mji wa Korogwe uliyopo wilaya ya Tanga.
Jaribu kujifunza historia ya nchi yako itakusaidia sana hata kupata mke au mme.
 
Hakuna mji wa Korogwe uliyopo wilaya ya Tanga.
Jaribu kujifunza historia ya nchi yako itakusaidia sana hata kupata mke au mme.
Umeniwahi,

Afu pia wala sio Kiungo cha kibiashara kati ya hizo sehemu alizotaja. Sema tu korogwe imepitiwa na barabara kuu iendayo moshi Arusha na Dar.

Hakuna wafany biashara wa hizo sehemu wanakuja kufungasha korogwe.

But nawasifia korogwe kwa gest nyingi afu Za bei chee
 
Unasema korogwe tu? Ungeanza na Handeni, huko ndio tatizo kwelikweli, Ukianzia na KABUKU, watu wanategemea maji ya kumvua kukinga kwenye paa la majumba, wanayatumia hata miezi kadhaa, siku ukiyaona ya Bomba ni mwezi Mara moja na nimachafu Kama maji ya barabarani, kwakweli nitatizo hasa, muheshimiwa Juma Awesu anakazi ya ziada.
 
Wakuu.

Mji wa Korogwe ambao upo Wilaya ya Tanga ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi sana na ni Mji kiungo kibiashara kati ya Lushoto, Tanga, Dsm, Moshi /Arusha, Morogoro....
Bora hata korogwe ina mito, Mwanza pale wana Ziwa kubwa kuliko yote Africa na Huduma ya maji yale haipo inapatikana kuleee kahama ,shy na Tabora
 
Shida ya Maji Tanga si Korogwe tu hata Muheza japo kuna ka unafuu muda huu lakini Handeni, Pangani na Kilindi pia Mkinga kote huko ni shida tupu
 
Unasema korogwe tu? Ungeanza na Handeni, huko ndio tatizo kwelikweli, Ukianzia na KABUKU, watu wanategemea maji ya kumvua kukinga kwenye paa la majumba, wanayatumia hata miezi kadhaa, siku ukiyaona ya Bomba ni mwezi Mara moja na nimachafu Kama maji ya barabarani, kwakweli nitatizo hasa, muheshimiwa Juma Awesu anakazi ya ziada.
Aweso si ni mbunge wa handeni?
 
Back
Top Bottom