Elections 2010 SHIBUDA vs KIKWETE; KURA UTAMPA NANI?

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Simaanishi kluwa kila mtu ni mfuasi wa CCM humu. lakini naomba kila mtu ajisikie huru kujibu.

Assume wewe ni Mjumbe wa NEC na majina mawili yameletwa kupigiwa kura kumpata mgombe uraisi kwa tiketi ya CCM. Kura ungempigia nani kati yao?

NB This is assumption as I believe even if CHIBUDA will apply for presidency, his name will not easily get passed for voting to the floor...
 
simpatii yeyote ya kwangu itaharibika
 
kwanini nipoteze kura yangu kwa watu hawa wawili? hata kama watapita urais mwaka huu, siwezi kuisaliti nafsi yangu kumpa kura hata mmoja wao kati ya hao....najua mwenyewe nani atachukua kura yangu mwaka huu.
 
naona wetu porojo nyingi mie kura yangu kama ningekuwa NEC
John Shibuda angechukua kura yangu
ikiwa nabadirisha nguo ikichafuka, vipi nisibadirishe raisi
akichemka?
 
Hilo si swali kwavile Shibuda hana nia ya kuchukua fomu ya urais alichofanya ni danganya toto ili ijulikana JK anweza kuwa na mpinzani,lakini Shibuda hatochukua fomu.
 
Hilo si swali kwavile Shibuda hana nia ya kuchukua fomu ya urais alichofanya ni danganya toto ili ijulikana JK anweza kuwa na mpinzani,lakini Shibuda hatochukua fomu.

hatachukua form? UNA MAANA KWAMBA ANAMWOGOPA SHEHE YAHYA aliyesema watakufa watakao fanya hivyo? nchi yetu inaongozwa na wachawi jamaniii!
 
Shibuda........... Kati ya vipofu, chongo ni mfalme. Mkuu kachemsha mbayaa... nchi imemshinda na mzigo wa fadhila umemuelemea
 
Ooooh! mimi nitampa Shibuda, mimi nitampa salim, mimi nitampa nani?, majority hamjajiandikisha kupiga kura na hata kama mmejiandikisha siku ya kura huwa hampigi. Wapiga kura wengi nchi hii wapo vijijini ambako huyo shibuda hajulikani. Subirini matokeo ambayo hamto-yapenda. "Mnataka kwenda peponi lakini kufa hamtaki, utakwenda vipi peponi kabla ya kufa"
 
Ni mchawi yupi anaongoza nchi? na kama yupo umejua vipi kuwa huyo ni mchawi? kwa vitendo vipi? au ni dhana tu?

mchawi ninayemwongelea ni shehe yahya, hii si dhana, kila mtu anajua kuwa uyu jamaa ni mchawi, mganga wa kienyeji, msoma nyota, mwiba nyota za watu, na ndiye viongozi wengi wanajivunia yeye kama ndo mchawi wao. nililokuwa nanliongea hapa ni kwamba, yeye alisema mtu atakayekuwa mpinzani wa kikwete atakufa, ndo nilikuwa nasema jamaaa ndo anaogopa kufa au?....by the way, kama kiongozi anaenda kwa mganga wa kienyeji mchawi msoma nyota, kigagula ili apate uongozi kichawi (as you know shetani ndo anatawala dunia hii ya uovu baada ya kumnyang'anya madaraka adam kwasababu ya dhambi, zamani sisi ndo tulikuwa watawala, sasa unless umeokoka ndo utatawala, kama haujaokoka uko chini ya shetani),...kama viongozi wanaenda kuchukua uchawi kwa mganga wa kienyeji ili watuongoze, kimahesabu ya kawaida ni kwamba, yule mchawi/mganga ndo anayeongoza nchi, kwasababu ndo anayemkontro yule kiongozi anayetuongoza. Unamjua shehe yahya?
 
Back
Top Bottom