IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
zumbemkuu nadhani sasa inatosha hata wale tuliokuwa na uvumilivu kwake sasa tunasema imetosha.
Ni muhimu sana shibuda akarudishwa huko magambani alikotoka, kuliko kumuacha atumie majukwaa ya chadema kukitukana chama chetu.
CHADEMA bwana yani issue ya shibuda ndio mnaiundia tume ambayo itagharimu fedha za walipa kodi kwa kitu kilicho wazi kabisa,fanyeni tu maamuzi magumuCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.
Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.
Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.
Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.
Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.
Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.
Source:Tanzania Daima
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.
Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.
Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.
Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.
Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.
Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.
Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.
Source:Tanzania Daima
mfukuzeni tu, but litazameni kwanza kisheria.
Wadau,
Hili andiko la bwana joseph limeenda skuli sana hebu tulipitie bila jazba.
MBUNGE wa Maswa Mashariki na mwanachama asiye wa siku nyingi wa Chadema, John Shibuda, amejikuta katika mtafaruku na wenye chama chao, kwa linaloitwa kosa la kutangaza kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Kinachowauma Chadema kupitia Baraza lake la Vijana (Bavicha) chini ya Mwenyekiti John Heche, ni kwanza kujitangaza kwa Shibuda mapema, pili kujinasibu kwamba atamwomba
Rais Jakaya Kikwete awe Meneja wake wa kampeni, lakini tatu mahali alikotangazia.
Bavicha wanalalamika Shibuda kutangaza azma yake hiyo katika semina ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Dodoma, lakini wanaloliona baya zaidi ni aliposema kwamba hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza Dola kama CCM.
Hapo ndipo wanapotamka wazi, kuwa kama anaona hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza Dola huku kila chama kikiwania kushika Dola, basi na aende katika chama anachoona kina uwezo huo, ambacho kwa mujibu wa Shibuda ni CCM.
Chadema wana haki ya kujibu pigo hilo la Shibuda, hasa pale ilipoona kama inabezwa kuwa si
miongoni mwa vyama vyenye uwezo wa kushika Dola, huku kikijinasibu kuwa ndicho kinachoelewa matatizo ya wananchi na kimbilio lao, lakini pia mpaka kikaonya dhidi ya
wanaotaka kukizuia kushika Dola mwaka 2015.
Pande hizi mbili za mgogoro huu zina haki ya kimsingi, kwamba Shibuda ana haki zote za kutangaza azma yake kama Mtanzania huru lakini mwanachama wa chama kinachojinasibu kujenga demokrasia na maendeleo kwa mujibu wa jina lake.
Lakini Chadema nayo ina haki ya msingi ya kujitetea, ili isidharauliwe wala kutibuliwa mipango yake ya kutwaa madaraka na kumsimamisha mgombea inayemtaka, ingawa hata
alichokifanya Shibuda kinaweza kuirahisishia kupata mgombea wake.
Ila kilichofanywa na Bavicha kumshambulia Shibuda, kinaonesha wazi kuwa demokrasia ndani ya Chadema ni ya hatihati, na huenda kuna wateule wachache ndani ya chama hicho wanaojua nani atagombea muda ukifika ni kinyume cha Demokrasia.
Tumeshuhudia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye ni mwanachama wa siku nyingi, Kabwe
Zitto, akisakamwa ndani ya Chadema pale alipotangaza kwamba urais anautaka na muda mwafaka ukifika atagombea.
Tulipata kushuhudia alivyosakamwa Zitto alipotaka kugombea uenyekiti wa Chadema dhidi
ya Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe; lakini ilikuwa vivyo hivyo kwa marehemu Chacha Wangwe, alipoonesha nia ya kugombea pia nafasi hiyo huko nyuma.
Chadema inataka kutwambia nini sisi ambao tulidhani kweli inajenga demokrasia sawa na jina lake? Inataka kutueleza kuwa ni ya wateule wachache na ndiyo wenye haki ya kugombea uongozi wa juu wa Taifa hili? Kwa nini iwe nongwa kwa wengine kujitangaza?
Mimi nadhani Shibuda hajakosea kiasi hicho kama ambavyo Bavicha inataka kuufahamisha umma, yeye alionesha nia na kuitangaza, ambalo si kosa katika Katiba ya chama chochote
achilia mbali ya nchi.
Kutangazia mbele ya wajumbe wa NEC ya CCM nalo si tatizo, kwa sababu Shibuda hakwenda pale kama mwanachama wa CCM, bali mjumbe wa Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Afrika (APRM) ambao ndio ulikuwa umeandaa semina ile kwa wajumbe wa NEC.
Shibuda kumwomba Rais Kikwete awe Meneja wake wa Uchaguzi nayo ni hiari yake kwa sababu kwanza ni mtani wake, lakini pia wakati huo Kikwete atakuwa amemaliza muda wake wa uongozi na kubaki kuwa Rais mstaafu, ambaye yawezekana kabisa hatakuwa na kikwazo.
Badala ya Chadema kumlalamikia Shibuda kwa uamuzi wake huo alioutangaza uwe mzaha, utani au uliodhamiriwa kwa dhati ya moyo wake, ungemtumia kujitangaza na kujenga uhusiano chanya na vyama vingine vya siasa vinavyoamini katika ujenzi wa demokrasia nchini.
Lakini pia kinapaswa kuwapa uhuru wanachama wao kutangaza azma zao mapema na hivyo kupata fursa ya kuona ni nani pumba na nani mchele, badala ya kubana fikra za wanachama katika kutoa hisia zao.
Chadema mlimpokea Shibuda kwa nderemo, vifijo na vigelegele alipohama CCM mkamsaidia mpaka akapata ubunge, iweje anapotaka urais mnaanza kumletea mikingamo na mizengwe na kuamini kuwa si afaaye?
SOSI: HabariLeo | Lipi kosa la Shibuda katika medani hii?
Msaidieni badala ya kumkatisha tamaa.
Wadau,
Lakini pia kinapaswa kuwapa uhuru wanachama wao kutangaza azma zao mapema na hivyo kupata fursa ya kuona ni nani pumba na nani mchele, badala ya kubana fikra za wanachama katika kutoa hisia zao.
Msaidieni badala ya kumkatisha tamaa.
Vizuri wanaunda kamati kwanza chini ya Prof. Safari; Shibunda ni kiongozi wa Sura Mbili hatakiwi kuongoza nchi
Kumvua uanachama haihitaji huko. tunaangalia katiba ya chama inasema nini kuhusu wajinga wajinga kama hao!
Watakao takiwa kuangalia sheria ni bunge baada ya kuvuliwa uanachama na kubaki uchi.
sikubaliani na shibuda ila napinga kufukuzwa//////mpuuzen////wekeni watu wa chini wamshughulikie kisiasa///viongozi wa kitaifa wa cdm wasijibishane naye////jimboni mwaketafuten watu compitent...waandaen//kuchukua jimbo///tambo za shibuda ni mizizi yake jimbon////mkienda naye papara kwa siasa za mihemko.///atawaacha majeruhi,,,,atavuruga chama//mnampa umaarufu////katumwa huyo//mtaona atatangaza hata bungen kugombea urais kupitia chadema/////kuwachanganya watu na kubadili upepo//////:spy: