Shibuda, CCM na kauli za utumwa - "...Muda wa vyama vya upinzani kukabidhiwa madaraka haujafika" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda, CCM na kauli za utumwa - "...Muda wa vyama vya upinzani kukabidhiwa madaraka haujafika"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Mwandishi Maalum Mwanahalisi - Imechapwa 23 May 2012

  [​IMG][​IMG]
  Uchambuzi


  HIVI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza vipi kujifananisha na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kulinda na kuheshimu demokrasia?


  Mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakiri leo hii hatuna hata chembe ya ubavu wa kujifananisha na CHADEMA ambacho tumeshikia bango la kukichafua.

  Ninaandika haya baada ya kuona jitihada za kupindisha ukweli, kuhusu kauli za John Shibuda, mbunge wa Maswa Magharibi kupitia CHADEMA.


  Shibuda amenukuliwa akisema, “…muda wa vyama vya upinzani kukabidhiwa madaraka haujafika.” Alisema hivyo Ian Smith, mlowezi wa Zimbabwe, lakini uhuru ulikuja haraka kuliko miaka 1,000 aliyotaka; na “utumwa” ukafutiliwa mbali.


  Lakini mtu anasema haya kwa gharama gani? Kwanza ni matusi kwa wananchi wanaotaka mabadiliko na kwa CHADEMA inayoongoza harakati hizo za kisiasa.


  Nilikuwa mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao cha CCM mjini Dodoma, ambamo Shibuda alitangaza kuwania urais mwaka 2015. Alivyoalikwa na alichokisema, ni yeye na viongozi wakuu wa CCM wanaojua.


  Katika mkutano huo, ndimo nilimsikia akitoa kauli za kudhalilisha CHADEMA; chama ambacho anasema anataka kukitumia kupata urais. Sasa kinachonisikitisha ni viongozi wa chama changu (CCM), kutoa kauli za kutetea kilichofanywa na Shibuda.


  Huyu anasema CHADEMA inamsakama Shibuda pasipo sababu; sababu ya kusakamwa kwake eti ni kwa kuwa “yeye hatoki Kaskazini.” Anaendelea, “…wasimbague Shibuda…Wasitafute visingizio vya kuondoa hoja hii na kumnyanyasa…” Hii ni kauli hatari. Ni dhambi ya unafiki.


  Shibuda huyuhuyu ambaye CCM inataka kubeba sasa, ndiye aliyesukiwa zengwe hadi kuondoka CCM na kujiunga na CHADEMA. Shibuda mwenyewe ni shuhuda.


  Mara kadhaa alizuiwa kugombea nafasi za juu za uongozi, ikiwamo mwenyekiti wa Wazazi. Kwenye urais pia, hata kama alikuwa anatania tu, jina lake lilikatwa na Kamati Kuu (CC).


  Katika maisha yake ya kisiasa ndani ya CCM, Shibuda hatasahau kilichompata mwa mwaka 2002 alipokuwa anakwenda Dodoma kwenye mkutano wa chama chake.


  Akiwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM, uliojumuisha pia uchaguzi, alishushwa kutoka garimoshi mjini Tabora. Kauli iliyotolewa wakati ule dhidi ya kitendo hicho, ni kwamba eti alikuwa anakwenda Dodoma “kuchafua viongozi wa juu wa chama – CCM.”


  John Malecela aweza kuwa shuhuda muhumu wa kilichopo ndani ya chama chake. Yeye mwenyewe amezuiwa kugombea urais mwaka 2005. Hakuzuiwa na vikao vya chama. Ni wakati wa uenyekiti wa Benjamin William Mkapa.


  Hadi sasa, hakuna kiongozi hata mmoja aliyeeleza sababu za Malecela kutogombea urais. Hata mwenyewe anasema hajaelezwa kilichomuondoa kwenye kinyang’anyiro hicho. Hii ndiyo “demokrasia?”


  Thomas Nyimbo, ni shuhuda pia wa kinachotendeka ndani ya CCM. Tangu mwaka 2002, Nyimbo amekuwa akizuiwa kugombea uongozi. Katika uchaguzi mkuu wa chama mwaka 2007, Nyimbo alijitosa katika kinyang’anyiro cha uenyekiti mkoani Iringa. Alienguliwa na vikao vya chama.


  Mwaka 2005 akajitosa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimboni Njombe Magharibi. Akashinda kura za maoni ndani ya CCM. Lakini wenye chama wakamuengua.


  Ushuhuda mwingine ni upatikanaji viongozi kati ya CHADEMA na CCM. Katiba ya CHADEMA inasema, “Kila mwanachama mwenye sifa ya kugombea nafasi yeyote anaruhusiwa kufanya hivyo,” zikiwamo nafasi za mwenyekiti, katibu mkuu, makamu mwenyekiti, naibu katibu mkuu – bara na Visiwani.


  Ndani ya CCM, Katiba inazuia baadhi ya nafasi kugombewa. Kwa mfano, hakuna anayeruhusiwa kugombea uenyekiti wa chama ngazi ya taifa. Hivyo hakuna mwanachama anayeweza hata kutamka maneno “…nataka kugombea uenyekiti.”


  Jina la mgombea mwenyekiti huletwa na “wenye chama,” kisha hupelekwa mkutano mkuu kuidhinishwa. Kazi ya mkutano mkuu ni kupiga kura ya ndiyo au hapana kwa jina lililoletwa. Basi!


  Mwenyekiti wa chama ndiye “anayeumba;” pia makamu wenyeviti wawili – Bara na Visiwani. Akimaliza kazi ya kuumba hupeleka jina la mhusika kwenye NEC. Kazi ya NEC ni kuidhinisha uteuzi wa mwenyekiti. Hakuna kuhoji. Je, udikteta huu, ndiyo viongozi wanaoita demokrasia?


  Naye katibu mkuu na naibu wake wawili – Bara na Visiwani – “huumbwa” na mwenyekiti. Yeye ndiye anateua kwa kupeleka majina yao kwenye NEC ili kuidhinishwa. Kazi ya NEC ni kuidhinisha matakwa ya mwenyekiti. Hakuna kuhoji wala kujadili.


  Ndivyo mwenyekiti wa sasa, Jakaya Kikwete alivyomuumba Yusuph Makamba mwaka 2007 na Wilson Mukama mwaka 2011. Mithiri ya kimbunga.


  Kabla ya Makamba kukabidhiwa ukatibu mkuu, Philip Mangula ndiye alikuwa anashikilia nafasi hiyo. Bila udikteta wa mwenyekiti, Mangula angeweza kuendelea kutumikia wadhifa wake huo hadi Oktoba 2007 ulipofanyika mkutano mkuu wa uchaguzi ili kukamilisha kipindi chake cha pili cha miaka mitano.


  Hata wajumbe wa CC hakuna anayeruhusiwa kugombea. Ni uteuzi wa mwenyekiti. Yeye ndiye anayechomoa majina kutoka miongoni mwa wajumbe wa NEC na kuyapeleka kwa wajumbe ili wayapigie kura.


  Kazi ya NEC, ni kupigia kura jina moja kutoka majina matatu ya wagombea walioletwa na mwenyekiti. Je, uteuzi huu nao unaweza kuitwa demokrasia ya uchaguzi?


  Ushuhuda mwingine, ni anguko la aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM), makamu wa rais wa Jamhuri na makamu mwenyekiti wa CCM Visiwani, Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1984.


  Alivuliwa nyadhifa zake zote za chama na serikali katika muda wa kufumba na kufumbua na tena ndani ya kikao cha chama chake. Hili amelieleza vizuri katika kitabu chake – The Partnership (Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, miaka 30 ya dhoruba). Uk. VIII.


  Kimsingi siyo kosa kwa Shibuda kutamani urais. Siyo kosa pia kutamkia maneno hayo kwenye mikutano ya CCM. Aweza kutoa kauli yake popote pale, hata kwenye klabu ya pombe.


  Nafasi ya CHADEMA katika siasa za sasa nchini inaeleweka. Ndicho chama pekee kilichosalia katika utetezi wa rasilimali za taifa. Ndio kimbilio la waliopoteza matumaini katika utawala wa miaka 50 wa CCM. Huu ni ukweli mchungu kwetu wana-CCM wote.


  Kuruhusu mtu kuvuruga CHADEMA sasa, kwa kukizushia tuhuma za uwongo, ni kutaka kuwarejesha wananchi kwenye utumwa. Baadhi yetu hatuko tayari kubeba dhambi hiyo.


  Bali Shibuda anaumwa. Ugonjwa wake ni huu: Ukosefu wa uwezo wa kupima athari ya kauli zake kabla ya kuzitamka. Anapenda sifa. Anataka aonekane mwanasiasa makini kuliko aliowakuta upinzani. Huu ni ugonjwa hatari. Nashangaa chama changu kupalilia ugonjwa badala ya kuutibu.   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Aende Zanzibar alikolelewa akawaeleze hayo!
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sana sana analeta mmomonyoko kwenye chama, hana lolote aliongeza acha muda wake uishe aende zake huko!
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Shibuda anataka Urais kwa chama cha CHADEMA lakini hapo hapo anasema CHADEMA kama Chama cha Upinzani hakifai

  kuongoza nchi, hayo yalisemwa na Ian Smith wa then Rhodesia (now Zimbabwe).

  Aligombea Uongozi mbalimbali ndani ya CCM - CULT na waliondoa Jina au walimshusha ndani ya Treni; na hakusema

  Chochote, unaona CCM ilivyo ni CHAMA CHA KIMAFIA - CULT; Hakujali wewe kama sio Mmoja wao au mtoto wa kwao

  * Sasa hivi Anacho fanya Kikwete kuajiri Vijana na kuvunja Umafia ndani ya CCM ni kuiua CCM, hajui anadhani hao Vijana

  Watamsaidia, hapana Vijana hawajui Undani wa CCM - Mafia Cult
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Umesoma hii habari hapo Juu? Jinsi CCM walivyombagua na CCM haikufa, CHADEMA haiwezi kufa sababu ya huyu Mmomonyoko Mmoja tu... amka
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kigeugeu
   
 8. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  cdm haiwezi yumbishwa na shibuda....... kama waziri mkuu alisha sema cdm inawanyima usingizi itakuwa huyo aliyefadhiliwa na cdm baada ya kutemwa na magamba
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Tayari Heche alishasema kwa mara ya 2 tulipokuwa pale viwanja vya jangwani(CHADEMA SQUARE) kuwa BAVICHA hatutamvumilia mtu yeyote atakayetaka kukivuruga chama, vijana wote waliunga mkono kauli hiyo pale pale tena kwa kumtaja jina, pia kamanda john mrema naye akapigilia msumari kauli hiyo kisiasa watu wakaitikia tena, pia Kamanda wa anga naye akapigilia msumari na ukumbi mzima wakaunga mkono kauli, sasa nadhani kama shibuda ataendelea na ujinga wake atakua anajisumbua bure.

  Peoples.....!
   
 10. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  R. I. P Shibuda, chadema imekushinda, rudi kwenye kichaka chako CHAMA CHA MAGAMBA.
   
 11. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ni kati ya mada ambazo nasema zinarudiwarudiwa hapa JF kama vile tuliomo sio ma great thinkerz kwakweli, embu leteni constructive topic sasa tupunguze na tofauti zetu sasa khaaa!
   
 12. B

  Blessing JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shibuda amechanganyikiwa he is not normal. Unajua anakunya na kukanyanga mwenyewe. Ni mswahilian kwa hivyo taabia yake is betraying him. Mie naomba afukuzwe kabisa ndani ya Chadema na kama anataka aende mahkamani. SHIBUDA NI MJINGA AVAI NDANI YA CHAMA naona ndio maana hata CCM wamemfukuza.

  AMETUMWA HUYO ----- AMEKATIWA POSHO YAKUHARIBU M4C lakini sisi wa PEOPLES atutingishiki wala atubabaishue na mtu. We are moving forward. PEOPLES, PEOPLES POWER THAT'S OUR MOTO.
   
Loading...