Shibuda: CCM imejaa wachumia tumbo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Na Samwel Mwanga, Shinyanga
MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejaa viongozi ‘wachumia tumbo' ambao hawana muda tena wa kufanya kazi ya kutekeleza ahadi yao ya kuwatumia wananchi.

Akihutubia wananchi juzi kwenye viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini hapa, Shibuda alisema kuwa CCM inaongozwa na wanyonyaji, hivyo akamtaka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nassoro Rufunga, kuacha tabia ya kutumia madaraka yake kuwatisha wananchi hasa wanaoshabikia vyama vya upinzani.

Shibuda alisema tabia ya Rufunga ya kuweka mbele suala la ‘ukada' wake wa CCM wakati wa kutimiza wajibu wake ni la hatari, na kumtaka aelekeze fikra zake katika kuwatumikia wananchi wa mkoa wake sambamba na kuwaondolea kero zinazowakabili.


Alielezea kusikitishwa kwake na taarifa alizopewa na wananchi kwamba pamoja na Rais Jakaya Kikwete, kuwapelekea mkuu mpya wa mkoa badala ya yule aliyestaafu, Brigedia Jenerali Dk. Yohana Balele, lakini mkuu huyo mpya ameonesha dalili za wazi za kukitumikia zaidi CCM badala ya wananchi.


Shibuda aliongeza kuwa pamoja na kwamba wakuu wa mikoa ni wajumbe katika kamati za siasa za CCM lakini wanapaswa kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao vya siasa na kwamba kinyume chake itakuwa ni uvunjaji wa Katiba ya nchi na viapo walivyoapa.


Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema mkuu wa mkoa hapaswi kutoa vitisho vya aina yoyote kwa wafuasi wa vyama vya upinzani kwa vile anapaswa kuwatumikia wote kama Watanzania na walipa kodi katika nchi hii.


"Kwa kweli nimesikitishwa sana na taarifa kwamba mkuu wetu mpya wa mkoa amekuwa akijisifu kuwa yeye ni mmoja wa makada wazuri wa CCM, lakini mimi naamini kufanya hivyo anakosea na kama ni kweli basi anavunja kiapo chake pale alipoapishwa na Rais Jakaya Kikwete.


"Sidhani kama anaielewa vema CCM, kama ni kweli aliyasema hayo niliyoelezwa ni vizuri basi akaitisha mdahalo kati yake na mimi ili tuweze kukaa na kuizungumzia CCM kwa undani kuliko anavyofanya hivi sasa, haielewi CCM kama mimi ninavyoielewa," alisema kuongeza:


"Leo hii CCM halisi haipo bali imebaki CCM ya wachumia matumbo, si kwa ajili ya kuwatumika Watanzania. Aandae mdahalo awakusanye na makada wengine wote kuanzia makatibu kata, makatibu wa wilaya na kamati nzima ya siasa waje tuelezane, tuwape nafasi wananchi waweze kuelewa ni yupi kati yangu na yeye anayeielewa vema CCM," alijigamba.


Mbunge huyo alisema kuwa muda wa Watanzania kutishwa hivi sasa haupo, bali kinachotakiwa ni utekelezaji wa ahadi walizoahidiwa wakati wa kampeni za uchaguzi si vinginevyo.



 
shibuda wewe ndo mchumia tumbo no 1. Hv umesahau kuwa hii serikali inaongwa na chama gani? Na inatekeleza sera ya chama gani? Subiri na nyie cdm muongoze mtafanya mambo yenu, usiwe mnafiki wa kuuma huku na kule tunakufahamu vzr sana wewe.
 
mbona huna pointi zenye mashiko, naamini hujui unalosema!!!!!!
sioni mantiki iliyopo kwenye red hapo chini.

shibuda wewe ndo mchumia tumbo no 1. Hv umesahau kuwa hii serikali inaongwa na chama gani? Na inatekeleza sera ya chama gani? Subiri na nyie cdm muongoze mtafanya mambo yenu, usiwe mnafiki wa kuumahuku na kule tunakufahamu vzr sana wewe.
 
Back
Top Bottom