Shibuda azushiwa tuhuma nyingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda azushiwa tuhuma nyingine

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 26, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Shibuda azushiwa tuhuma nyingine

  Zulfa Mfinanga, Shinyanga na Frederick Katulanda, Mwanza

  HALI ya kisiasa kwenye Jimbo la Maswa Magharibi bado ni tete baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, John Shibuda kuachiwa huru na polisi kwa maelezo kuwa hakuhusika kwenye mauaji ya dereva wa gari la CCM, huku kamati ya maadili ya uchaguzi ya wilaya ikiandika barua kutaka kada huyo wa zamani wa chama tawala aenguliwe kugombea.

  Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuchunguza tuhuma za mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Robert Kisena kumshambulia na kumbwaga chini kamanda wa polisi wa wilaya, ikisema iwapo atabainika kuwa alihusika atafikishwa mahakamani.

  Watu wengine 11 wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema jana walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika kwenye vurugu dhidi ya wafuasi wa CCM zilizosababisha mtu mmoja kupoteza maisha.
  Shibuda na Kisena walikamatwa na polisi baada ya kutokea vurugu kubwa baina ya wafuasi wa Chadema na wa CCM karibu na eneo ambalo chama hicho cha upinzani kilikuwa kikiendesha mkutano wake wa kampeni za ubunge na vurugu zilisababisha dereva wa mgombea huyo wa CCM, Steven Kwilasa kupoteza maisha.

  Wakati Shibuda alifuatwa na polisi kwenye mkutano huo wa kampeni Oktoba 21 na kuwekwa ndani tangu Oktoba 21 akituhumiwa kuhusika kwenye vurugu zilizotokea takriba kilomita moja kutoka sehemu alipokuwa, Kisema alikamatwa Jumapili akituhumiwa kumshambulia kamanda hyo kwa mateke akiwa kituo cha polisi. Alihojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa huru.

  Afisa mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Shinyanga, Seleman Nyakipande ambaye pia ni mjumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza vurugu hizo inayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, aliiambia Mwananchi kuwa Shibuda ameachiwa kwa dhamana jana jioni.

  Alisema kuwa Shibuda alikidhi masharti yote ya dhamana aliyowekewa na kwamba kwa sasa yupo huru na kuongeza kuwa moja ya masharti aliyopewa ni kupatikana wakati atakapohitajika na jeshi hilo.

  “Kwani jana tulivyozungumza nilikwambiaje, si nilisema Shibuda anaweza kuachiwa siku na muda wowote; sasa tulishamwachia kwa dhamana jana jioni ila tutakapomuhitaji asikosekane,” alisema Nyakipande.
  Akizungumza na Mwananchi jana, Shibuda aliwashukuru viongozi wa CCM kujaribu kumuhusisha na tuhuma za mauaji akisema kuwa njama hizo zitamuongezea kura Oktoba 31 mwaka huu.

  Shibuda alidai kitendo cha katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba kufika wilayani Maswa na kushindwa kwenda kumuona akiwa mahabusu, kinaonyesha kuwa kada huyo wa chama tawala si mkomavu wa siasa na kwamba bado amejaa chuki na hasira baada ya kukihama chama.

  Shibuda alisisitiza kauli yake ya awali kuwa kukamatwa kwake kulitokana na shinikizo la baadhi ya viongozi wachache wa kisiasa ambao walitaka kutumia msiba kama mtaji wao wa kisiasa kujijenga, lakini akasema lengo lao limekwama.

  “Msiba huu umetokea si kwa sababu ya masuala ya itikadi za vyama. Mimi ninaamini kabisa kuwa mauaji haya yametokea kutokana na msukumo wa mtu binafsi na wala siyo itikadi za vyama. Nimeliomba Jeshi la Polisi lichunguze kwa makini kwa vile chanzo kipo na hatua zichukuliwe,” alieleza.

  Alisema ukiangalia kwa uhakika hali inajionyesha wazi kuwa aliyekwenda kufanya vurugu hakutumwa na chama chake kufanya hivyo awe wa CCM ama wa Chadema, bali kutokana na msukumo wa akili ya mtu na hivyo kuwaomba watu kutofautisha mizozo ya itikadi za vyama na mizozo ya akili za watu binafsi.

  Shibuda, ambaye alionekana mwenye furaha, alisema kuwa amefurahisha na hatua ya polisi kufanya upembuzi wa haki na wa kina na kuamua kumwachia huru kwa vile imani yake ni kuwa kukamatwa kwa awali kulikuwa na shinikizo la kisiasa ambalo liliandaliwa na baadhi ya viongozi chama kimoja.

  Alisema kuwa kwa vile ameachiwa basi shinikizo hilo la kumuweka ndani kwa misingi ya kiasiasa limemuongezea umaarufu ambao utawafanya wananchi kumpigia kura za huruma hivyo kuibuka na ushindi mkubwa zaidi kuliko aliokuwa akiutarajia awali.

  Lakini kamati ya maadili ya wilaya inataka mbunge huyo wa zamani wa Maswa kwa tiketi ya CCM aondolewe kwenye orodha ya wagombea ubunge wa mwaka huu baada ya kutuma barua ya mapendekezo kwenye kamati ya maadili ya taifa kuitaka iiondoe Chadema kushiriki katika uchaguzi.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa, Elizabeth Kitungu alisema kuwa kikao hicho cha mapendekezo kilifanyika Jumamosi na barua kutumwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) jana na kuongeza kuwa tayari Chadema wameshaandika barua ya kujitetea kupinga kuondolewa katika kinyang'anyiro hicho.

  Mkurugenzi wa uchaguzi wa Nec, Rajab Kiravu alisema kwamba hajaipata barua inayotoa mapendekezo hayo, aliahidi kutoa taarifa za mchakato mzima wa suala hilo na nini kitakachofuatia.

  Akizungumzia hatua hiyo ya kamati ya maadili, Shibuda alisema hilo ni jambo ambalo haliwezekani na kuwashauri wasimamizi kuwa wasithubutu kufanya hivyo kwa vile yeye hajathibikika kutenda kosa lolote linaloweza kumvua sifa ya kuwa mgombea.

  “NImesikiasikia, lakini mie nasema kamati ya maadili ya jimbo haina mamlaka ya kunijadili na kuniwekea pingamizi kwa jambo hili la mauaji na wala hawawezi kuniwekea pingamizi na kama walikuwa wakifikiria kufanya hivyo, waache mara moja,” alisema Shibuda.

  Shibuda alisema kwa kipindi ambacho alikuwa anashikiliwa na polisi ametambua imani yake kwa wananchi wa jimbo hilo na mapenzi yao kwake kwa vile walikuwa wakimfariji na kuvipongeza vyombo vya habari vilivyoandika kwa umakini jambo hilo na kuvilaani vile ambavyo viliandika kwa malengo ya kupotosha na kugeuza ukweli.

  “Hata taarifa za kuwekewa pingamizi zimeandikwa na baadhi ya magazeti kwa misingi ya kutaka kugeuza ukweli; hivi navilaani sana, lakini wawashukuru waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi na wale wa kitaifa ambao walifuatilia kwa kina jambo hili na kuhakikisha haki inatendeka,” aliongeza Shibuda.

  Wakati huohuo, watu 11 wanaohusishwa na tuhuma za kufanya vurugu na kusababisha kifo walipandishwa kizimbani jana mbele ya hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, hakimu Thompson Mtani.

  Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Naipenda Mwananchi inaandika vizuri, jambo hili, siku ya kwanza ya tukio la kuua waliwahoji wagombea wote waliohusika katika vulugu, walimhoji Shibuda na Kisena, walimhoji OCD aliyepigwa na RPC wake akajibu pumba. Angalia na leo wamemhoji Shibuda baada ya kutoka na msimamizi wa uchaguzi anayetaka kumwengua shibuda kwa shinikizo la CCM. walau ukisoma unapata kitu hebu soma Mtanzania loooooooooooooooooo!
   
Loading...