Shibuda ampokea Kikwete Dodoma

Kwa ziara ya kiserikali mbunge wa upinzani kumpokea Rais ni sahihi, lakini kwa hii ziara ya kichama mbunge wa upinzani hapaswi kuwepo pale, ila kwa Shibuda siwezi kushangaa maana yeye ni mwanaccm alieingia Bungeni kwa tiketi ya CHADEMA, kwa wale wanachama wa CHADEMA NI LAZIMA MKUBALIANE NA UKWELI HUU.
Cha kumshukuru Shibuda ni kwamba ameboost kidogo kwenye fungu la ruzuku ya chama na idadi ya wabunge wa CHADEMA, lakini kwa itikadi yeye ni CCM. HUU NDIO UKWELI.
 
Me sioni tatizo kwani siasa ni vita? acheni mawazo ya kijuha.
 
jinsi walivyosaliminiana ni exactly namna freemasons wanavyoshikana mikono wakisalimiana,siamini aisee!
 
Wadau hili la shibuda kwenda kumpokea Kikwete limekaaje?hili nao nafikiri ni Gamba lingine.

View attachment 41723
Nadhani hili ni suala binafsi, yawezekana walikuwa na appointment ili wazungumzie masuala yao binafsi kama ya kifamilia na kadhalika, plz naomba tusiliangalie hili kwa jicho la kisiasa.
 
Sikujuaga kwamba Shibuda siku hizi ni Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini!
Hata kama Shibuda angekuwa ni mbunge wa Dodoma mjini lakini hakupaswa kuwepo pale, ile ni ziara ya kichama ya JK, PALE WA KUMPOKEA NI MKUU WA MKOA KWA SABABU NI KADA WA CCM, NA VIONGOZI WOTE WAKUU WA CCM.
Ila msisahau huenda kulikuwa na nyama pale ndicho kilichompeleka pale Shibuka maana msukuma yule ana uchu balaa.
 
Ni kweli mleta thread jaribu kuiweka sawa hii thread yako..maana tunaweza kuchangia kitu ambacho si sahihi..tuambie alimpokea wapi? kwenye nini? na lini? ukitupa hayo majibu nadhani tutachangia kwa uwazi zaidi...
 

WeWE NDO MSHAMBA,Umeshndwa kujua kuwa JK yuko kichama huko dodoma? Shibuda anajipendekeza,hafai kuwa kiongozi,wananchi watashndwa kujua msimamo na muelekeo wake.a leader has to show a direction and be at the front,sasa yeye anawaelekeza wapi watu? Wewe unayeita wenzio washamba utakuwa kibarua wa magamba.
 
Huyu Shibuda ni wa kumdharau tu! Hana aibu huyo hapo bila kuzuiwa anaweza hata kuingia kwenye vikao vya CCM!
 
Maana ya siasa si uhasama. Siasa za vyama vingi ni kutumia njia za amani na usalama mnapohitilafiana ili kufikia malengo.

Vita ndiyo uhasama.

Sera za "upiganaji" toka lini zikawa ni siasa? Nawashangaa sana wasajili wa vyama wanachokiwacha chama chenye sera za "upiganaji" kuendelea kupata usajili.

Shibuda ni mwanasiasa na si "mpiganaji".
 
Jamani mjadala huu unatakiwa uongezewe picha nyingine ya gazeti la mwananchi hapo ndipo tuanze mjadala baada ya kumpokea (tz daima)alimvuta pembeni kumnong'oneza(mwananchi)tuanze mjadala
 
Acheni unafki JF, mtendeeni haki huyo Shibuda na Chadema, hapo ni ndani ya uwanja wa ndege na siyo kwenye mkutano wa wabunge wa CCM, someni magazeti ya leo
 

Hapo naona mzee Msekwa hakuipenda hiyo move, halafu naona kwenye picha kuna ndugu wawili wa damu, mmoja aliwekewa nazi baada ya kuzaliwa bila kichwa , na huyo wa mtera aliwekewa dafu baada ya kuzaliwa bila kichwa, baba mmoja mama mbali mbali.Halafu kwa mbaali naona yule chapombe anakenua kama m/kiti wake.
 

Kweli kabisa. Siasa sio uadui ni kazi kama kazi nyingine. Kwani ukihamia kampuni moja nyingine ndo unaachana na washikaji wa mwanzo? Ushamba huo.
Shibuda yuko sahihi kabisa.
 
Shibuda, Drogba wa siasa za bongo, kama alivyowahi kusema baada ya kurudi tena bungeni. Hapo sio anampokea Kikwete. Yuko kiwanjani anafanya mavitu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…