GE2025 Shetta: Tuilinde amani yetu kwa wivu Mkubwa Kwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 tukachague viongozi bora kutoka CCM

GE2025 Shetta: Tuilinde amani yetu kwa wivu Mkubwa Kwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 tukachague viongozi bora kutoka CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram Mgombea Udiwani kata ya Mchikichi Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Nurdin Bilal Juma (Shetta) ameandika:

"Tuilinde amani yetu kwa wivu mkubwa ndugu zangu watanzania !
Kwa kujitokeza kwa wingi tarehe 29 oktoba tukapige kura kwa amani tukawachague viongozi bora, na viongozi bora wanatokana na chama cha mapinduzi. Tusifanye makosa"



1759139706236.png




 

Attachments

  • 1759140439033.png
    1759140439033.png
    1.9 MB · Views: 16
Wendawazimu na wanafiki ndio watajitokeza kwenye hayo maigizo.
 
Kiutani utani mara Sheta Mbuwe mara waziri wasomi jitokezeni tofauti na hapo mtaongozwa na kina shetta mkubali wakosoaji wa JF wa Chama cha mapinduzi muingie huko mkiwa wapinzani
 
Gama ya bongo fleva imemkataa kila akijaribu kurudi anashindwa, naona ameamua kuingia kwenye uchawa
 

Ifike mahali watu wasikwepe uwajibikaji katika kivuli cha kuilinda amani.

Nchi nyingi zilizoingia katika machafuko basi lazima kiwepo chanzo watu mamilioni kwa pamoja hawawezi wote kuwa wendawazimu.

Nimeweka kipande cha video hicho kwenye mradi unaogharamiwa na walipa kodi halafu bado wanadandia kama nyani , madirishani ni hatari kiusalama na hata kwa afya ya akili.

Mwananchi amekamuliwa tozo na kodi bado anadandia gari la umma kama nyani halafu anasikia leo kuna mtoto wa kiongozi amelipa bilioni 2.4 kwa ajili ya vigae,unafikiri mtu huyu atakuwa na amani?

Mimi sichukii utajiri ila ninaamini katika utajiri halali , mfano leo hii ukiniambia Benjamin Fernadez ni bilionea siwezi kushangaa sababu huyu mtu katoa solution fulani kusaidia tatizo katika jamii ambayo ni program ya kitanzania ya kwanza inayowezesha watanzania kutuma pesa wakiwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa gharama nafuu .

Sasa tuje kwa huyu bilionea wa mchongo na dili kupitia uongozi wa mzazi wake amewahi kutoa huduma gani kijami iliyokuwa ni suluhisho?

Jibu ni kuwa hajafanya uvumbuzi wowote au huduma yoyote iliyotatua tatizo kwenye jamii hivyo hakuna mahali inaweza kuthibitishwa uhalali wake na ndio maana wahusika waliichomoa risiti ile mapema sana kwenye kanzidata yao.

Hitimisho machafuko yana chanzo, niliwahi kuona makala fulani kuhusu DRC kijiji kiligundulika kina madini mwisho wa siku wanakijiji wakatimuliwa na serikali ikaingia kuchimba ajabu watu wanaachiwa mashimo ya migodi na magonjwa huku huduma za kijamii zikizorota matokeo yake ikageuka vita na eneo likawa halitawaliki maana wananchi hawaoni faida ya uwepo wa madini katika eneo lao.

Hivyo hao kina Shetta sijui Shetani wawajibike ninaamini Chalamila na kitambi chake hawezi kudandia mwendokasi hivyo badala yake anakula kiyoyozi katika gari ambayo kodi analipa anayedandia hapo mwisho hapo hakuna usawa na suala la amani litakuwa na walakini na kulazimishana.
 
Back
Top Bottom