Shetani kafa?

Shetani kafa?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,341
Reaction score
15,829
wanajamvi yaani siku hizi binadamu anavyofanya mambo ya kikatili huwezi dhani kama ni kiumbe chenye akili timamu...mara mtu kasepa na kichwa cha mtu,mara mkono wa mtu,mara vichanga vimebakwa,mara hawa wameuana kwa kudhulumiana,mara tembo wanaisha wakati watu waliapa kulinda maliasili...mara..........yaani utafikiri tumeambiwa shetani kafa so hakuna jehanam....au kafa? Mbona hatuogopi
 
Sio kafa, amezaa na sasa ndo yuko kwenye full control yeye na wadogo zake akina Kapuya.
 
ana wajukuu kabisa!! ila mzee mwenyewe ndo anapga dili kubwa kubwa kama za kina kapuya.
 
Haaaa mwingine jana alisema mungu kafa !! Mbona hamsaidii , kila analoomba hamsaidii ,, ila mi naona shetani sasa kaamua kuifanya kazi yake sawasawa kwa kututumia sisi viumbe zaifu !! Mara tindikali , mapanga ,na anautumia udhaifu wetu ipasavyo.
 
na wewe nae mtanzania?
 
Logic gani unatumia?

Kama shetani ndiye baba wa maovu na mungu ndiye baba wa mema, na maovu yanazidi, swali la kuuliza hapa lingekuwa "mungu kafa?" si "Shetani kafa?".

Kwa sababu shetani anaonekana kufanikiwa sana kwa mujibu wako, mfu hawezi kufanya kazi kwa ufanisi hivi.

In any case, habari nzima za shetani na mungu ni za kusadikika zaidi, zisizo na uthibitisho.

Waswahili walisema, ibilisi wamtu ni mtu.

Shetani na mungu wanasingiziwa tu.
 
Logic ndogo tu... kama nyumbani kwa mfano baba ndiye anayeonekana mtu anaeogopwa na watoto wanaogopa kufanya maovu kwa sababu yake, akifa si ndio wanaanza kujiachia? Maana Mbingu haiogopwi bali Jehanam...Au mkuu hujawahi sikia familia ambazo watoto wameharibikiwa baada ya mdingi kudedi?
 
Naona sh*t*ni katuzidi akili mpaka tunaanza kufikiria kafa. Badla cc wenyewe tunatakiwa tubadilike..mm nadhani cc binadamu ndo chanzo bhana.
 
Jehanamu moto umezimika na kile kimbunga ambapo mabaki yake yaliangukia ufilipino juzi kati,kwa hiyo ni full kujiachia kamanda,iba,tapeli,baka,ua,piga,zini,loga,sodomize na lewa kwa kwenda mbele,tuko huru!
 
Unajua kuna dhambi binadamu tunazifanya mpaka shetani mwenyewe anashangaa! lakini ukiona hivi ujue jua ndio linazama!
 
Logic ndogo tu... kama nyumbani kwa mfano baba ndiye anayeonekana mtu anaeogopwa na watoto wanaogopa kufanya maovu kwa sababu yake, akifa si ndio wanaanza kujiachia? Maana Mbingu haiogopwi bali Jehanam...Au mkuu hujawahi sikia familia ambazo watoto wameharibikiwa baada ya mdingi kudedi?

Kwa logic hiyo basi swali lingekuwa kama mungu kafa, si kama shetani kafa.

Kwa sababu mungu ndiye anayetakiwa kuwa anasimamia kutofanya maovu na watu wanatakiwa kuogopa kufanya maovu kwa sababu yake.

Sasa watu kama hawaogopi kufanya maovu tena, swali ni "Mungu kafa?".

Swali haliwezi kuwa "Shetani kafa?" kwa sababu kwa mujibu wa thread hii kazi ya shetani inaendelea vizuri sana, na ya mungu inadorora.

Aliyekufa hawezi kufanya kazi yake vizuri.

Kwa hiyo swali hapa ni "Mungu kafa?" na wala si "Shetani kafa?".

In the context of this thread.
 
Imeandikwa,jinsi wakati utakavyokuwa unayoyoma na siku za shetani kuitawala dunia utapokuwa unakwisha basi shetani atalitambua hilo na kuongeza nguvu zaidi ili kufanikisha kuwa na idadi kubwa ya wafuasi wake. Wachache wenye imani thabiti ndio watakaopata fursa ya kutambua haya. Haya yataambatana na wingi wa manabii wa uwongo watakao kuwa na miujiza mikubwa na ya kutisha wakitumia jina lile lile ya Yesu. Wengi wataamini. Magonjwa ya kutisha na yasiyo na tiba. Tumrudie Mungu ili tupate ufunuo wa nyakati hizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom