Hujaeleweka unakubaliana na mawazo yangu au tunatofautiana?Kusoma biblia kikasuku unaweza kuchanganyikiwa au kutaka kusafiri bila paspoti.
Nimekubali kutokukubaliana nawe.Hujaeleweka unakubaliana na mawazo yangu au tunatofautiana?
Akikuelewa na aikane nafsi yake. Hiyo ni mumo kwa pale!😂😂😂... jambo moja ( kwa hayo maandiko) tuna hakika nalo; walikula lile tunda walilokatazwa. Swali, mbona hawakuwa kama Mungu? Mbona hawakufa?
Jamaa someni kwa kuelewa na si kufuata nadharia za watu wengine.... jambo moja ( kwa hayo maandiko) tuna hakika nalo; walikula lile tunda walilokatazwa. Swali, mbona hawakuwa kama Mungu? Mbona walikufa?
Huoni kwamba Shetani aliwaingiza chaka? Logic rahisi hivi nayo ni ngumu kueleweka? Makubwa utaelewa kweli?
Mkuu sasa kwani kabla ya kula haya Matunda walikuwa wanakufa?Kwani kabla ya kula hayo matunda walikuwa hawajui mema na mabaya?Kwani shetani yeye aliwahi kula hayo matunda?Unaposoma maandiko yoyote kabla ya kuhitimisha jiulize Maswali.Shetani hakumdanganya Hawa na Adam kama baadhi ya viongozi wa dini na baadhi ya wapendwa katika dini wanavyosema na kumlaumu katika ibada zao isipokuwa shetani alimwambia Hawa ukweli.
Shetani alimwambia Hawa ukweli ambao Mungu hakutaka Adam na Hawa waujue. Katika bustani ya Eden Shetani/Ibilisi(nyoka) alimwambia Hawa mambo makuu mawili;
1. Wakila matunda waliyokatazwa watakuwa kama Mungu.
2. Wakila matunda waliyokatazwa hawatakufa.
Nikianza na jambo la kwanza, Shetani alimwambia Hawa kuwa wakila matunda ya mti waliokatazwa basi watakuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya.
Kweli baada ya Adam na Hawa kula matunda waliyokatazwa walipata maarifa ya kutambua mema na mabaya na kufikia hatua ya kujitambua kuwa wako uchi na kuanza kujifichaficha. Mpaka hapa hakuna uongo uliosemwa na shetani. Rejea (mwa 3:1-12).
Katika jambo la pili, Mungu baada ya kugundua Adam na Hawa wamekula matunda aliyowazuia, wamepata maarifa na wamekuwa kama yeye kwa kujua mema na mabaya aliamua kuwafukuza kutoka katika bustani ya Eden ili wasije kujiongeza tena wakatwaa matunda ya mti wa uzima wakala wakaishi milele. Hii ina maana Shetani hakudanganya kwa maana Adam na Hawa wangefanikiwa kula tunda la mti wa uzima wasingekufa na wangeishi milele na hii inaonyesha shetani hakuwa muongo. Mungu mwenyewe anathibitisha hili jambo katika (mwa 3: 22-24)
Kwa kuzingatia hayo mambo wawili inaonyesha si kila kitokacho kwa shetani ni uongo au ni jambo baya kwa binadamu mana bila nyoka kutimba bustanini huenda binadamu bado angekuwa zezeta asiye na maarifa yoyote lakini pia bila Mungu kuingilia kati huenda binadamu tusingekuwa tunawaza kuhusu kifo na kupata majonzi ya kufiwa na wapendwa wetu mana tungeishi milele. Tafakari
Una hoja.kusadikika
Msingi wa hoja zetu ujikite katika mada kuu kwa kuzingatia vifungu vya biblia nilivyo nukuu na si kuleta hoja za jumla. Ukitumia hoja za jumla huwezi pata maana halisi ya nukuu hizo.Mkuu sasa kwani kabla ya kula haya Matunda walikuwa wanakufa?Kwani kabla ya kula hayo matunda walikuwa hawajui mema na mabaya?Kwani shetani yeye aliwahi kula hayo matunda?Unaposoma maandiko yoyote kabla ya kuhitimisha jiulize Maswali.
Issue kubwa kwenye simulizi hii ni utii.Ni kukosa imani kwamba Mungu aliyetuumba au aliyewaumba Adamu na Eva na Nia njema na ni Mwema.Ni kuamini kwamba Mungu alikuwa na Sinister Agenda dhidi ya Binadamu aliyomuumba.Ni mbegu ya Shaka,wasiwasi ambayo shetani aliipanda.
Aliipanda kwanza kurudia Maelekezo ambayo Mungu Aliwapa Adam na Eva na kumuaminisha Eva naye Eva kumuaminisha Adam kwamba Huyu Mungu sio mwema kama ambavyo anatuaminisha.Kosa lile ambalo lilimuangusha Ibilisi ndilo ambalo lilimuangusha Adamu.
So Always Shetani anachokwamba ni Muongo na ni Baba wa Uongo.Shetani kamwe hasemi ukweli wowote ULE
Ukitumia common sense utadhani huu ni ujuaji. Ila ukitumia critical sense utapata maana ya huu uzi.Ujuaji mwingi huleta madhara makubwa tafakari
Soma uzi kwa umakini na vifungu nilivyonukuu utaona moja ya miongoni ya miti ya matunda waliokatazwa ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya pamoja na mti wa uzima.Uongo +ukweli = Uongo
Ukweli + Uongo = Uongo
Ukweli + Ukweli = Ukweli
Uongo +Uongo = Uongo
Shetani aliongea Uongo Kwa sababu hakusema kweli yote.
Kama shetani alisema ukweli kama usemavyo, tuambie aadamu na Hawa wapo nyumbani kwako tuje kuwaona?
Au Babu yako mzaa Babu yupo?
Ni kweli Mungu ni mweza wa yote kwa mujibu wa maandiko.Huenda Mungu alimtuma Shetani ndio maana Eva alikubali. Kumbuka Mungu Ni mweza ya yote.
Ni kweli mana kabla ya ukoloni haya mambo hayakuwepo mababu zetu walikuwa na taratibu zao huko nyuma.Wazungu wasinge tutawala nafikiri hata sisi tungeweka hadithi zetu kwenywe kitabu kimoja, sadiki na chitemo , Juma na uledi , mutegeki na nyembo, akili na adili, chilunda apambana na chui , Lindu ampiga kampilima, chunguza na maua , asiye sikia la mkuu, androko na simba , fuata nyuki ule asali , na nk.