mara nyingi Serikali inapeleka Muswada wa sheria Bungeni ukiwa tayari umeandaliwa kisomi na mabingwa wa sheria pale wizara ya katiba na sheria kwa ushirikiano na ofisi ya mwanasheria mkuu na kwa kupewa mwongozo wakitaaluma kutoka katika taaluma husika inayotungiwa sheria, mfano sheria ya wanyamapori,ni lazima kuwe na kamati ya wanataaluma hiyo ambao wao wataclear all doubts za kisomi ndani ya fani husika, na kamati hiyo ya kitaaluma/technical staff inakutanaga na wadau wa sekta husika kupata maoni yao, kisha muswada huo ukiishakupitiwa na mkundi yote ndio hupelekwa kwenda kupitishwa na wabunge, kwa ujumla ofisi ya mwanasheria mkuu ndo inapaswa kuwajibika kama sheria husika hakukidhi haja, na hapo wabunge watasema walipotoshwa na ofisi hiyo, kama ambavyo Chenge anavyolaumiwa leo.