Sheria ya Utumishi wa umma No.2 ya 2002 inawatambua wakuu wa wilaya/mikoa kama watumishi wa umma

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Ni kifungu namba 5(1)(d),unaweza pia kudownload katika mitandao,wahakikiwe wenye vyeti,wavionyeshe,na pia,iangaliwe namna ya kuwahakiki wasio na vyeti,watafutwe wataalam wa kuthibitisha kama wanajua kusoma na kuandika.....uthibitisho ni sehemu ya uhakiki
Screenshot_2017-04-28-18-37-14.png
Screenshot_2017-04-28-18-37-27.png
 
Ila toka mwanzo nilisema na narudia kusema makonda hakuna wa kumuweza hata akifanya kosa la aina yeyote labda magu mwenyewe aamue watu mkanitukana ila leo mtakubaliana na mimi kwani mjadala umeshafungwa.
Tatizo ni katiba letu, kwanu hakuna wa kupingana na raisi. Na raisi yupo juu ya sheria.
Ni hekima na matakwa ya raisi ndio yanaendesha nchi.
Narudia makonda hawezekani
 
Ni kifungu namba 5,unaweza pia kudownload katika mitandao,wahakikiwe wenye vyeti,wavionyeshe,na pia,iangaliwe namna ya kuwahakiki wasio na vyeti,watafutwe wataalam wa kuthibitisha kama wanajua kusoma na kuandika.....uthibitisho ni sehemu ya uhakikiView attachment 502267 View attachment 502269
Sheria ulisoma chuo gani? Kwa mujibu wa sheria, Wakuu wa Wilaya na Mikoa SIO WATUMISHI WA UMMA; NI VIONGOZI WA UMMA.
 
Sheria ulisoma chuo gani? Kwa mujibu wa sheria, Wakuu wa Wilaya na Mikoa SIO WATUMISHI WA UMMA; NI VIONGOZI WA UMMA.
Mtu yeyote anayelipwa mshahara wa serikali kutoka HAZINA ni mtumishi wa umma.
Be serious mdau.
Mkuu wa wilaya na RC unasema si watumish wa umma wakat Katibu Mkuu Kiongozi anawasimamia pia
 
Mtu yeyote anayelipwa mshahara wa serikali kutoka HAZINA ni mtumishi wa umma.
Be serious mdau.
Mkuu wa wilaya na RC unasema si watumish wa umma wakat Katibu Mkuu Kiongozi anawasimamia pia
Usiingize siasa na matakwa yako katika kutafsiri sheria.... sheria haitafsiriwi kwa mihemko au matakwa ya mtu binafsi. Natudia tena - WAKUU WA WILAYA NA MIKOA NA VIONGOZI WENGINE WA KISIASA SIO WATUMISHI WA UMMA - NI VIONGOZI WA UMMA. Kinadharia Unaweza Kuwaona ni Watendaji wa Umma Ila Kisheria Hao Sio WATUMISHI wa Umma (PUBLIC SERVICE EMPLOYEES)... Naishia Hapa. Sitakujibu Tena.
 
Back
Top Bottom