Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
Wakati wakiwa bungeni waliishia kumneng'enekea mwenyekiti badala ya kufanya mabadiliko kwenye Sheria yatakayolinda haki ya kila mtu kuchaguliwa .

Kuwahurumia wanaccm ni sawa na kutojitambua tu kwa sababu wao ndiyo wajenzi wa huu uovu bila kujali hata kesho yao.
 
Back
Top Bottom