Sheria ya nguvu ya saikolojia

Sheria ya nguvu ya saikolojia

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,348
Reaction score
1,097
ONEKANA (STAND ABOVE) . Kazi nzuri huwa hazionekani. Kama unataka kuwa na nguvu zaidi kazi nzuri tu haitoshi . kufanya kazi sana tu haitoshi ila unatakiwa ufanye kazi huku ukitambulikana (UKIONEKANA ) .Kazi yako isiwe overshadowed . Pata muda kuongoza na kujihakikishia unaonekana. UKITAMBULIKANA NI RAHISI KUFANIKISHA HAYO MALENGO . Biblia inasema heri jina jema kuliko fedha na dhahabu Mithali 22:1.

FICHA DHAMIRI YAKO (HIDE YOUR INTENTION) .Kwa mfano unakwenda kununua gari . Muuzaji akiwa anaona ile dhamiri ya dhati ya kununua kwako ataweza kupandisha bei . Kwa nini anaweza kupandisha bei? Kwa sababu umempa nguvu ya maongezi (the power of conversation). Inatakiwa uonyeshe kama hutaki ili ile nguvu yako ya ndani uitumie. Yeye aanze kukushawishi. ANAYEKUSHAWISHI SIKU ZOTE HANA NGUVU, WEWE NDIWE MWENYE NGUVU. Watu wengi hii nguvu ya ndani huitosa. Ndiyo maana tunasema shetani hana nguvu.

MATENDO DHIDI YA MABISHANO (ACTION OVER ARGUMENTS). Unaweza ukabishana kwa kadri uwezavyo na kupata ushindi wa kufurahi nafsi. Bali ushindi wa mabishano huwa hakuna unachopata. Kupata nguvu ya kisaikolojia usitumie muda mwingi kubishana. Kama mtu anataka kubishana muache tu, ila wewe usibishane naye. Siku zote matendo huongea kuliko maneno.

ZINGATIA UNAYOONGEA (MIND YOUR WORDS) . Jinsi unavyoongea sana ndivyo mazungumzo yako au hotuba yako inakuwa haina maana. Ukiongea pale inapobidi tu, unakuwa unaongeza nguvu yako ya ndani ya kusema kwako hata Watu kutaka kukusikiliza zaidi. Tofauti na hapo huondoa ile heshima kutoka kwao. Ukiwa unaongea kwa uchache hata ukikosea hutaonekana kama umekosea.

TENGENEZA KUJIAMINI (CULTIVATE CONFIDENCE). Maisha yako ya nyuma siku zote yanakuangazia mambo matatu, vikwazo, kushindwa na kurudi nyuma. Nguvu yako ya kisaikolojia inaweza kupungua ndani yako hasa ukipata washauri wabaya. Watu wanaokata tamaa, huondoa nguvu hii ya kisaikolojia. Hivyo usikae na wakatisha tamaa. palilia kujiamini. Unafanyaje basi? hakikisha kila fanikio lako dogo lione kama ni kubwa na jipe moyo zaidi.

AJIRI ADUI ZAKO (HIRE YOUR ENEMIES). Marafiki ni wazuri katika maisha ila ni hatari katika muenendo wako wa mafanikio, kwani wanaweza KUIBA NGUVU YAKO YA NDANI. Kuna muda tunatia matumaini yote kwao na kuwaamini. don’t be blind sided by people whom you trust . Tusiwaamini sana wale tunaona tunawaamini Wanaweza kutupofusha . Badili uelekeo kwa kumchukua yule ambaye aidha unamuona haaminiki au ni adui yako . Kuna uwezekano mkubwa sana akakupa clear objectivity . ADUI yako anaweza kuonyesha UAMINIFU kwa sababu anataka kukuhakikishia ni muaminifu .

WATU NI WABINAFSI . Ili usipoteteze nguvu yako ya ndani . Kama unataka msaada usitegemee sana watu wawe kimsaada kwako . bali itokee tu . Watu wapo kukusaidia kama tu kuna kitu wanataraji kupata . Kama unataka watu wakuelewe na kukusaidia . Waambie kwa kufanya hivyo wao ndiyo watakaopata si wewe utapata . Wataanza kukuelewa .

EPUKA MAJUKUMU ( AVOID COMMITMENT) .Epuka ahadi na majukumu yasiyokuwa na tija kwa watu .majukumu huingiza watu katika shida . Watu wanakupenda upande huu na kukutega upande mwingine na kukufungia huko . Jukumu lako likianguka unaanguka nalo . Kama unataka kuwa na nguvu ya ndani kuwa na majukumu yanayoeleweka .Uwe na majukumu na wewe tu . kwa kufanya hivi utakuwa na majukumu na wote .

JISHUSHE ( PLAY YOURSELF DOWN ) . Kila mtu anataka kuonekana na akili .Kama unataka kuwapata watu, waonyeshe kuwa wao wapo vizuri kuliko wewe .ingawa unajijua ulivyo smart ila usionyeshe . Kujishusha hapa maana yake unaonyesha wewe si lolote kwake na huna cha kushuhudia . Watu huwa hawaangalii wewe ni mzuri kiasi gani ( how intelligent you are ) . Bali hujiangalia wao kuwa ni wazuri zaidi( more intelligent than others) . Watie moyo katika mambo yao waonyeshe kuwa wao ni bora sana . SIKU ZOTE UNATENGENEZA MAADUI KWA USEMA WEWE NI BORA SANA ZAIDI YA WENGINE .

WASAIDIE WALIO KUZIDI( SUPPORT YOUR SUPERIOR ) . Siku zote ukipanda ngazi lazima uheshimu ngazi iliyokupandisha . Usiende kinyume kwa waliokuzidi na kuwaona si kitu kwa mafanikio uliyopata . Kuwa bega kwa bega na boss wako . Ukifanya hivyo atakupa recommendation nzuri kwa maboss wenzake na watu wote wakuu . Hata kama umefanya wewe mpe tuzo mkuu wako kuliko wewe .

KUWA MAKINI SEHEMU MOJA ( STAY CONCENTRATED IN ONE PLACE) . Kupata nguvu ya kisaikolojia usiangalie tu nguvu uliyo nayo pekee .Watu wengi wanaweza kufanya mambo mengi kwa wakati . Hata inapelekea kuhamia fani moja kwenda nyingine , Wanajikuta si wataalam wa fani yoyote ( they have not specialized in anything ) . Kuwa na fani moja yenye nguvu ya kukamatia , uwe hapo .

TAFAKARI NAMI .
 
Hakika ni chakula safi cha ubongo
 
Maisha ambayo napenda kuyaishi kila siku.

Hakuna raha kama mtu kajiandaa kubishana alafu wewe unamuambia "basi ndugu tumalize hili jambo mimi nakubali wewe uko sahihi"

Kama upo kwa watu wengi basi wewe ndo utaoneka uko smart zaidi ya yule jamaa anayevimba,na roho yako itakuwa na amani muda mfupi baadae.
 
Pole sana. Na hongera najua kukopi kitu mtandaoni na kukitafsiri sio kazi ya kitoto.
 
Shukrani sana japo maisha au hata mafanikio hayana formula wala ujuzi ni mixture ya matokeo
 
Back
Top Bottom