Sheria ya Makosa ya Mitandao inatumika kwa watumiaji wa mitandao wa ndani ya nchi tu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,516
2,000
Kama mtandao haujasajiliwa Tanzania,Jamuhuri ina haki na nguvu za kisheria ku-demand taarifa za watumiaji wa mtandao ambao umesajiliwa nje ya nchi?

Msingi wa swali langu ni kutokana na uelewa wangu mdogo katika maswala ya sheria kwamba Sheria ya Makosa ya Mitandao inatumika kwa watumiaji wa mitandao wa ndani ya nchi na mitandao /blogs zilizosajiliwa hapa nchini tu.

Ukitumia mtandao kama wa facebook kufanya makosa ya mtandao na ukajulikana wewe ni fulani na ulifanya kosa hilo ndani ya ardhi ya Jamuhuri ya Muungano bila shaka huwezi kusalimika kwasababu unatumia jina lako halisi(unafahamika) na zaidi unakuwa umetenda kosa hilo ndani ya Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano(sina uhakika sana kama Sheria hii ya Makosa ya Mitandao ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili iweze kutumika upande wa Tanzania visiwani pia)

Swali:

Anaetumia ID fake na akiwa ndani ya Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini usajili wa uanachama wake katika mtandao husika umefanyikia online nje ya nchi,Sheria hii ya Makosa ya Mtandao inaweza kumbana mmliki wa mtandao huo kutoa taarifa za mtumiaji wa mtandao husika ili hali server za mtandao huo zilizotumika kumsaji mtumiaji huyo zikiwa ziko nje ya nchi wakati nje ya nchi Sheria hii ya Makosa ya Mtandao haitumiki?

Wanasheria tunaomba mtusaidie hapa.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,031
2,000
Mkuu hawatafanikiwa mashitaka yao yote ni Batili....

Kesi wataichelewesha lakini mwisho lazima washindwe tu......

Lengo lao ni kumsumbua tu ndugu yetu lakini ukweli ni kuwa hawana hoja ya maana kumtia kizuizini...

Wanatekeleza ajenda yao ya kutumiwa na wanasiasa......
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,516
2,000
Kama mtandao haujasajiliwa Tanzania,Jamuhuri ina haki na nguvu za kisheria ku-demand taarifa za watumiaji wa mtandao ambao umesajiliwa nje ya nchi?

Msingi wa swali langu ni kutokana na uelewa wangu mdogo katika maswala ya sheria kwamba Sheria ya Makosa ya Mitandao inatumika kwa watumiaji wa mitandao wa ndani ya nchi na mitandao /blogs zilizosajiliwa hapa nchini tu.

Ukitumia mtandao kama wa facebook kufanya makosa ya mtandao na ukajulikana wewe ni fulani na ulifanya kosa hilo ndani ya ardhi ya Jamuhuri ya Muungano bila shaka huwezi kusalimika kwasababu unatumia jina lako halisi(unafahamika) na zaidi unakuwa umetenda kosa hilo ndani ya Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano(sina uhakika sana kama Sheria hii ya Makosa ya Mitandao ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili iweze kutumika upande wa Tanzania visiwani pia)

Swali:

Anaetumia ID fake na akiwa ndani ya Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini usajili wa uanachama wake katika mtanda husika umefanyikia online nje ya nchi,Sheria hii ya Makosa ya Mitandao inaweza kumbana mmliki wa mtandao huo kutoa taarifa za mtumiaji wa mtandao husika ili hali server za mtandao huo zilizotumika kumsaji mtumiaji huyo zikiwa ziko nje ya nchi?

Wanasheria tunaomba mtusaidie hapa.
Petro E. Mselewa tusaidie hapa
 
Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Ndiyo maana wanawataka wamiliki wa mitandao wote wasajili mitandao yao hapa nchini (watumie domain ~co.tz). Ili Sheria Iwabane na iwe rahisi kuidhibiti mitandao hiyo.
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,475
2,000
Mkuu Salary Slip, nashukuru kwa kuthamini uelewa wangu katika mambo ya kisheria. Kimsingi, vyombo vya usalama vina mamlaka ya kutaka na kupatiwa taarifa za watumiaji na wamiliki wa mitandao ya simu, ya kijamii na kadhalika. Kikwazo kikubwa kilichopo JF ni kuwa taarifa zake hazipatikani hapa Tanzania. Hivyo, Max Melo asingeweza kuwapatia taarifa hizo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom