Sheria ya kurithi wajane katika Biblia

Sheria ya kurithi wajane katika Biblia

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Wasalaam wana JF.
Nimekuwa nikifuatilia kujua asili ya utaratibu wa mjane kurithiwa na ndugu wa marehemu mumewe.Nimegundua kuwa utaratibu huu kumbe ni wa miaka mingi sana tokea enzi za nabii Mussa!
Nanukuu Maandiko.matakatifu kutoka kitabu cha kumbukumbu la torati.
"Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.
Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.
Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu"
Kumbukumbu la Torati 25 :5-10

Mbarikiwe sana
 
Na ilikua kwa ambaye hajazaa watoto ila kwa aliyezaa mke hakurithiwa
 
Back
Top Bottom