Sheria ya kumpata Spika ibadilishwe kabisa

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Jinsi tulivyoshuhudia upatikanaji wa spika wa bunge hapa Tanzania haipendezi kwani kila siku atatoka kwa wabunge waliowengi Bungeni, hali ambayo inanyima haki kwa wachache.

Tumeshuhudia Bunge la Anna Makindi lilivyokuwa la hovyo kwa kuangalia wengi wanasema nini, na ndicho kilicho igharimu CCM katika uchaguzi huu, hadi wakaanza kutumia mbinu za wizi wa kura bila hivyo wangeshindwa kabisa, kwani wananchi walikuwa na hasira sana na wabunge wa CCM kwa kuitetea serikali hata pale inapo haribu, mawaziri mizigo wanaachwa tu.

Sasa nawashauri safari hii wasipobadilika yatawakuta makubwa zaidi mwaka 2020.
Ushauri:- Kama Spika Atapatikana kwa wabunge waliowengi basi Naibu apatikane kwa wabunge walio wachache ili kubalansi huduma.
kama Magufuli anapenda haki sawa ili asiteseke mwaka 2020 basi anaweza kushauri ili sheria hiyo ibadilishwe.
 
Jinsi tulivyoshuhudia upatikanaji wa spika wa bunge hapa tanzania Haipendezi kwani kila siku atatoka kwa wabunge waliowengi Bungeni, hali ambayo inanyima haki kwa wachache, Tumeshuhudia Bunge la Anna Makindi lilivyokuwa la Hovyo kwa kuangalia wengi wanasema nini, na ndicho kilicho igharimu CCM katika uchaguzi huu, hadi wakaanza kutumia mbinu za wizi wa kura bila hivyo wangeshindwa kabisa, kwani wananchi walikuwa na Hasira sana na wabunge wa ccm kwa kuitetea serikali hata pale inapo haribu, mawaziri mizigo wanaachwa tu. Sasa nawashauri safari hii wasipobadilika yatawakuta makubwa zaidi mwaka 2020.
Ushauri:- Kama Spika Atapatikana kwa wabunge waliowengi basi Naibu apatikane kwa wabunge walio wachache ili kubalansi huduma.
kama Magufuli anapenda Haki sawa ili asiteseke mwaka 2020 basi anaweza kushauri ili sheria hiyo ibadilishwe.

Huwezi kuchagua kiongozi wa mhimili nyeti kama huo kwa kigezo cha uchache na wingi.
 
Spika hapaswi kua mwanachama wa chama chochote kile. Bunge ni mhimili mkuu wa nchi sio chama. Katiba mpya ni muhimu sana.
 
Mbona ndugai ccm na huyo sijui tuliani naye kisha pewa Ubunge na ccm ili akipendelee chama chake kweli hii si haki kabisa magufuli naomba ujitahidi ili tushangaike 2020 siy ombali
 
Jinsi tulivyoshuhudia upatikanaji wa spika wa bunge hapa Tanzania haipendezi kwani kila siku atatoka kwa wabunge waliowengi Bungeni, hali ambayo inanyima haki kwa wachache.

Tumeshuhudia Bunge la Anna Makindi lilivyokuwa la hovyo kwa kuangalia wengi wanasema nini, na ndicho kilicho igharimu CCM katika uchaguzi huu, hadi wakaanza kutumia mbinu za wizi wa kura bila hivyo wangeshindwa kabisa, kwani wananchi walikuwa na hasira sana na wabunge wa CCM kwa kuitetea serikali hata pale inapo haribu, mawaziri mizigo wanaachwa tu.

Sasa nawashauri safari hii wasipobadilika yatawakuta makubwa zaidi mwaka 2020.
Ushauri:- Kama Spika Atapatikana kwa wabunge waliowengi basi Naibu apatikane kwa wabunge walio wachache ili kubalansi huduma.
kama Magufuli anapenda haki sawa ili asiteseke mwaka 2020 basi anaweza kushauri ili sheria hiyo ibadilishwe.
Unashauri unatishia unafoka.kwa mujibu wa mabunge ya jumuia ya madola,kanuni ya wengi wape ndio inaongoza,kwa hiyo subiri 2020
 
Huduma gani unataka iwe balansi???, kwani taratibu za kuchagua spika huzijui????? wacha taratibu zifuatwe
 
Bunge linahitaji viongozi wenye weledi na wasiopendelea upande wowote. Bungeni huwa na pande mbili kubwa,yaani upande wa chama tawala na ule wa upinzani. Spika na Naibu Spika ndio viongozi wa Bunge ukiachilia mbali Wenyeviti wa Bunge.

Mfumo wa sasa wa kumpata Spika na Naibu Spika ni mfumo wa kichama. Mfumo uliopo hauwezi kukwepa upendeleo. Mfumo uliopo,uliobarikiwa na Sheria zitumikazo,unataka wagombea wa Uspika na Unaibu Spika wawe wamefadhiliwa na vyama vya siasa. Ndiyo kusema wagombea lazima wawe wanachama wa vyama vya siasa na kupitishwa navyo.

Katika namna hiyo ya kuwapata viongozi hao wa Bunge,Bunge litaendelea kuwa lililosheheni upendeleo wa wazi na hata wa kificho kwa upande anaotokea Spika. Ifike mahali viongozi hao,iwekwe kisheria kabisa,wasitokane na vyama vya siasa.

Natumai Wabunge watashughulika na masuala ya katiba mpya,sheria mpya na hata Tanzania mpya.
 
Bila katiba mpya itabaki kuwa ndoto. Chamsingi tuwaambie wabunge wetu wa ukawa kazi kubwa tunayoomba watufanyie ni kutuletea katiba mpya, la sivyo tutachagua ccm 2020.
 
Cccm tena? are u serious? si bora usipige kura ujuwe moja?
 
Hivi hamna shughuli za kufanya na vipi kuhusu post zenu kabla ya gia ya angani? Petro ni looser Mara hana chama Mara. Hakuna mtu wakati , km sio CCM basi mpinzani. Hao walio neutral ndio kina kubenea
 
Bunge linahitaji viongozi wenye weledi na wasiopendelea upande wowote. Bungeni huwa na pande mbili kubwa,yaani upande wa chama tawala na ule wa upinzani. Spika na Naibu Spika ndio viongozi wa Bunge ukiachilia mbali Wenyeviti wa Bunge.

Mfumo wa sasa wa kumpata Spika na Naibu Spika ni mfumo wa kichama. Mfumo uliopo hauwezi kukwepa upendeleo. Mfumo uliopo,uliobarikiwa na Sheria zitumikazo,unataka wagombea wa Uspika na Unaibu Spika wawe wamefadhiliwa na vyama vya siasa. Ndiyo kusema wagombea lazima wawe wanachama wa vyama vya siasa na kupitishwa navyo.

Katika namna hiyo ya kuwapata viongozi hao wa Bunge,Bunge litaendelea kuwa lililosheheni upendeleo wa wazi na hata wa kificho kwa upande anaotokea Spika. Ifike mahali viongozi hao,iwekwe kisheria kabisa,wasitokane na vyama vya siasa.

Natumai Wabunge watashughulika na masuala ya katiba mpya,sheria mpya na hata Tanzania mpya.
Mkuu una hoja ya msingi kabisa. Nachelea kusema kubadili sheria ili Spika na Naibu wasitokane na vyama ni jambo gumu sana

Ni gumu kwasababu hakuna maadili wa uaminifu na hatuwezi kujua hata yule asiye na chama kama kweli hana chama

Nitakupa mifano

Jaji mkuu mstaafu wa JMT alichukua form ya Urais kupitia CCM. Nani alijua kabla kuwa ni mwanachama wa CCM?

Yule mwakilishi wa Udasa bunge la katiba tulijua ni mwana taaluma, kwani si umeona ?

Kuna yule Kijana tulijua anawakilisha NGO, leo si unaona ni kada mwaminifu wa CCM?

''Mwanasheria mdogo'' ambaye ni mtumishi wa umma, leo si unaona mambo ya 'voda fasta''

Kuna maprofesa wa taaluma, leo si unawajua ni makada maarufu tena wakitumia taaluma zao kuhadaa umma

Nadhani jibu la maana ni kuanza na katiba, na hili lianze sasa! bila hivyo ni ngumu sana
 
Haka kanchi bwana!Kana taka moyo kuishi,wananchi msipobadilika na kupaza sauti za kutaka katiba hamtakuja pata.
 
HIVI UKAWA WAMENYIMWA NAFASI YA KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE? mbona mnalalamika lalamika tu ka kuku anataka kutaga yai?
Yaani mahali ambapo democrasia inatumika ya wengi wape nyie mnapoona mpo kidogo, mnataka irekebishwe iwapendelee! Hii haitatokea, ni democrasia kwenda mbele, kila chama kitapata mgombea wao kivyao kisha watapambanishwa kwa kupigiwa kura!
 
Jinsi tulivyoshuhudia upatikanaji wa spika wa bunge hapa Tanzania haipendezi kwani kila siku atatoka kwa wabunge waliowengi Bungeni, hali ambayo inanyima haki kwa wachache.

Tumeshuhudia Bunge la Anna Makindi lilivyokuwa la hovyo kwa kuangalia wengi wanasema nini, na ndicho kilicho igharimu CCM katika uchaguzi huu, hadi wakaanza kutumia mbinu za wizi wa kura bila hivyo wangeshindwa kabisa, kwani wananchi walikuwa na hasira sana na wabunge wa CCM kwa kuitetea serikali hata pale inapo haribu, mawaziri mizigo wanaachwa tu.

Sasa nawashauri safari hii wasipobadilika yatawakuta makubwa zaidi mwaka 2020.
Ushauri:- Kama Spika Atapatikana kwa wabunge waliowengi basi Naibu apatikane kwa wabunge walio wachache ili kubalansi huduma.
kama Magufuli anapenda haki sawa ili asiteseke mwaka 2020 basi anaweza kushauri ili sheria hiyo ibadilishwe.

unataka ofisi ya Spika iwake moto? ukiweka watu wawili wa vyama tofauti kwa hali ya sasa, utasababisha moto tu hakuna litakalo fanyika.
 
Back
Top Bottom