Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 11, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on June 11, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Katibu wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Yahya Khamis Hamad

  SHERIA ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itawasilishwa kesho katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoanza kujadili bajeti ya mwaka wa fedha serikali ya mwaka wa fedha wa 2012/2013. Katibu wa baraza hilo, Yahya Khamis Hamad aliwaambiwa waandishi wa habari jana katika mkutano uliofanyika ukumbi wa baraza la wawakilishi, kwamba jambo la kwanza kuwasilishwa kwa wajumbe wa baraza ni sheria hiyo ambayo wananchi wanasubiri kuitolea maoni.
  “Hii itakuwa ni taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi ambayo ni kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kifungu 132 (2) ambayo inahitaji sheria zinazohusu muungano kuwasilishwa katika baraza” alisema Hamad.
  Hamad alisema katiba haitoi nafasi ya kujadili sheria hiyo kwani itakuwa ni taarifa kwa wajumbe wa baraza na sio kuijadili, “Hii ni kwa mujibu wa katiba lakini tusibiri litakaloweza kutokea baada ya kuwasilishwa sheria hiyo kwa sasa hatuwezi kujua nini kitatokea”.
  Katibu Hamad alisema sheria hiyo inawasilishwa katika baraza la wawakilishi katika kikao cha kesho kwa sababu ndicho kikao cha kwanza tangu bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitisha sheria hiyo.
  “Waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar Abubakar Khamis Bakari atatoa taarifa kuhusu sheria hiyo” alisema Katibu huyo.
  Akijibu suali la waandishi juu ya kuchelewa kwa kuwasilishwa sheria hiyo kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi, Katibu huyo alisema “Bado hatujachelewa kuwapa wajumbe taarifa kwa sababu hiki ndio kikao cha kwanza” aliongeza Hamad.
  Tangu kupitishwa na bunge sheria hiyo na kusaniwa na Rais Jakaya Kikwete ilitarajiwa tume ya katiba ingeanza kazi zake ya kukusanya maoni ya katiba mpya mwezi huu, hata hivyo kikwazo kikawa ni kutowasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kama gazeti hili lilipoandika hivi karibuni.
  Akizungumzia utaratibu wa kikao hicho ambacho ni bajeti ya pili tangu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Katibu alisema hakuna mswada mwengine utakaowasilishwa isipokuwa miswada ya kuidhinisha matumizi ya fedha za serikali.
  Alisema jumla ya masuali 197 yataulizwa na kupatiwa majibu na mawaziri wahusika ambapo tayari tayari matayarisho ya kikao hicho yameshakamilika ikiwemo wajumbe wote waliopo kisiwani Pemba kuwasili hapa Unguja.
  Tokea kuapishwa kwa wajumbe wa tume ya katiba Rais Kikwete wananchi wa Zanzibar wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na suala la kuwasilishwa sheria hiyo ya katiba katika kikao cha baraza la wawakilishi.
  Wazanzibari wengi wamekuwa na shauku kubwa wakitaka kujua kitakachotokea katika baraza hilo juu ya sheria ya katiba itakayowasilishwa na waziri wa katiba na sheria.
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Ikiwa Muungano hautakiwi itakuwa Katiba? huu Muungano umekuwa kama Mwanamkke Mala.. alakuwa hajuwi kufukuzwa na kukataliwa.

  Hebu Watanganyika mujitao Watanzania na kujinata muna kila rasilimali na makeke, hamujuwi kukataliwa? nyinyi nikungangangania tu, aibu tena kwenu .

  Kila Mtanganyika macho yamewatoka kuona Wazanzibar hawawataki, jee kwani kabla ya Muungano mulikuwa munaishi vipi?
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  povu jingi. Tumia na elimu ya darasani basi
   
 4. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,316
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  povu mnalo nyinyi tena la kule......maana humu kila mmoja roho juu

  Kila Mtanganyika macho yamewatoka kuona Wazanzibar hawawataki, jee kwani kabla ya Muungano mulikuwa munaishi vipi?
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Kakee ni kweli Muungano ni kama ndoa, Tanganyika ndio Bwana na Zanzibar ndio bibi, sisi wanaume wa bara hatuna utamaduni wa kuacha mke, tena mwanamke mwenyewe mzuri kama Zanzibar, kamwe hatuachi!.

  Hizi chokochoko ni visa vya mke kutingisha kibiriti ili ampime mumewe kama kweli anapendwa, huyo ni mke anayetafuta tuu mapenzi akiyapata kisawa sawa, atatulia!.

  Ila pia kuna aina ya visa vya mke aliyepata bwana mwingine!. Tumesikia fununu mmepata bwana mwingine wa Kiarabu ndio maana sisi machogo mnatuona hatuna maana hata baada ya kukutunza na kukuhudumia kwa kila kitu yapata miaka 48 sasa!.

  Maadam mshenga wenu BLW amekuja, dai basi hiyo talaka yenu tukupeni tuachane kwa usalama ila hala hala msije kujuta!. Msiache mbachao kwa msala upitao na siku zote, mkataa pema pabaya panamwita!. Msubirieni tuu mjukuu majuto!.
   
 6. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,316
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kwani hii ni ndoa au raping???
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Sio rape bali ni ndoa ya mkeka ambapo upande mmoja wa kidume Tanganyika ndio iliridhia kwa kuleta posa huko kupitia kwa mshenga Karume ambapo barua ya posa ilikubaliwa, japo mke hakuulizwa anataka mahari ya kiasi ili aridhie rasmi kuolewa na Tanganyika bali ndoa ilifungwa rasmi ile tarehe 26 April, 1964, na tarehe 27 April, 1964, mshenga Karume alimleta rasmi mke na kumkabidhi kwa Tanganyika pale Karimjee!.

  Kisheria ndoa ya upande mmoja sio halali ila ili kuibatilisha ilibidi mke aliyeolewa bila ridhaa yake, kugoma kutimiza masharti ya ndoa ile ikiwemo kutotoa huduma za kindoa hivyo kuonyesha kuikataa ndoa ile batil!.

  Kitendo cha mke kujituliza tuli ndani ya ndoa, hiyo ndoa ikawa "consumated" na mpaka leo mke hajaomba rasmi kutoka ndani ya ndoa ile, ni uthibitishi kuwa yule mke aliiridhia ndoa ile kwa kukaa kimya hivyo ndoa hiyo kupata uhalali kwa kutumia "the law of limitation".

  Kukubali kwa kukaa kimya ni moja ya mila nzuri za Kiafrika kwa binti mwenye adabu njema kukaa kimya anapoombwa penzi ila ukimshika mkono kumpeleka chumbani huja bila kulazimishwa na mle ndani nguo huvua mwenyewe, kitandani alipanda mwenyewe na miguu pia alifungua mwenyewe!. Hivyo hiyo sio rape!.

  Hizi chokochoko za vile vitimbakwiri zinaketwa kwa sababu ametokea bwana wa kiarabu na kutaka kumfitinisha mke kwa kumkumbushia kuwa hawakupokea mahari!, eti yeye ataleta majunia ya dhahabu kama mahari!. Sasa hivyo vitimbakwiri ndivyo vinamchokoa dada yao aombe talaka ili wao wapate mali!.

  Kwa taarifa tuu dada yao kapenda kwa dhati, kajituliza kwenye ndoa hivyo fitina zao ni bure tuu!.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Duhh mimi ni mtanganyika, lakini naipenda sana Zanzibar. Sitakubali muungano uvunjike. Siku hizi hata usingizi sipati. Beautiful aisland of Africa
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali Tatu zitatatua migogoro
   
 10. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu tukiwa na serikali 3 haitatua migogoro kwa sababu wazenji wataanza kulalamika kwamba serikali ya muungano inaipendelea serikali ya Tanganyika (kumbuka sasa kwamba huu utakuwa uke wenza), hivyo kusababisha kuendelea kuwa na kero zisizokwisha. Nadhani suluhisho sahihi na la kudumu ni Serikali moja au Kila mtu kushika lake.
   
 11. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sanga kwa hili sikubaliani nawe. serikali tatu zitsababisha muungano kufa maana kila serikali itajali mambo yake hivyo kusahau mambo ya muungano. Nafikiri serikali moja ndilo suluhisho la kunusuru ndoa hii
   
 12. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakubaliana na wewe 100%
   
 13. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wanaosema serikali tatu zitazidisha malumbano baina ya Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar; na hatimaye kuvunja Muungano. Kama serikali moja haitatakiwa na Zanzibar, basi ndoa itavunjika.

  Tujuavyo ni kwamba Wazanzibari kadhaa hawautaki Muungano na wamediriki hata kupeleka ujumbe Umoja wa Mataifa kuomba Umoja huo uingilie. Wengi wetu wa Bara tunadhani pia sio lazima tuwe na Muungano, na kwamba maendeleo yetu Tanganyika yangesonga mbele kwa kasi zaidi kwa kuachana na Zanzibar.

  Kwa hiyo Tume ya Katiba ipendekeze kura ya maoni kwa wananchi wa Zanzibar na kwa wananchi wa Tanganyika. Endapo mmoja kati ya Zanzibar au Tanganyika hataki Muungano, basi Tume iandike Katiba mbili: moja ya Tanganyika na ingine ya Zanzibar. Tusilazimishe upande wowote kuwa ktk Muungano.
   
Loading...