Sheria ya hali ya hatari nchini Sudan yapunguzwa muda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280

KHARTOUM,SUDAN
MUDA wa kutekelezwa sheria ya hali ya hatari nchini Sudan umepunguzwa kutoka mwaka mmoja na sasa ni miezi sita.



Taarifa zaidi zinasema kuwa, Bunge la Sudan lilitangaza kupunguza muda wa hali ya hatari kutoka mwaka mmoja na kuwa miezi sita.
Tangazo la Bunge la Sudan la kupunguza muda wa utekelezwaji wa sheria ya hatari ya hatari kutoka mwaka mmoja hadi miezi sita linatolewa katika hali ambayo, nchi hiyo imeendelea kukumbwa na maandamano dhidi ya serikali karibu kila siku.
Maafisa wa polisi nchini Sudan wameendelea kuzima maandamano ya wananchi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi, sanjari na kuwatia mbaroni viongozi waandamizi wa vyama vya upinzani.
Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitangaza kwamba watu karibu 60 wameuawa hadi sasa katika maandamano hayo.
Maandamano ya hivi sasa ya nchini Sudan ni makubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Maandamano hayo yaliyoanza kwa kulalamikia ughali wa maisha sasa yamebadilika na kuwa ni wimbi la kumtaka Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo ang’oke madarakani, lakini bado anashikilia msimamo wake wa kubakia madarakani.
 
Back
Top Bottom