China wanawajibikaje kuhusu mgogoro na machafuko ya Sudan

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,661
46,350
Kuondolewa madarakani kwa dikteta wa muda mrefu wa Sudan, Omar al-Bashir mwaka 2019 hakukusaidia nchi hiyo kujikwamua kutoka katika misukosuko na machafuko yake ya kisiasa ya muda mrefu.

Sasa vikundi vya kijeshi vinavyotawala nchi viko katika mapigano makali ya kuwania madaraka. Hata hivyo haya yote yamekuwa yakiendelea huku China ikitanua na kukita zaidi ushawashi wake katika taifa hilo la Kiarabu. Kwa sasa China inamiliki 75% ya uwekezaji wote wa mafuta nchini humo na imeikopesha nchi hiyo zaidi ya bilioni 10$.

Kama ingekuwa ni US au taifa lingine la West wako Sudan katika hali kama hii wangetupiwa kila aina ya lawama kwamba wanahusika na huo uharibifu na vurugu, ila hatuoni China wakitupiwa lawama hizi au wakitakiwa kuwajibika kuleta amani Sudan kwa sababu ni wazi katika hali kama hii ya machafuko na serikali kukosa udhibiti kiwango kikubwa cha mafuta kitakuwa kinaibwa na kutoroshwa kutoka Sudan na wawekezaji.
 
China yeye muuwane mtajua wenyewe yeye anajichotea mali na kuzidi kuwakopesha pesa.
 
Ukishasema china ana maslahi Sudan sharti umuweke marekani kwenye equation,kugawanywa Sudan ni kazi ya marekani,mafuta mengi yapo Sudan kusini miundombinu ya kuyanywa hayo mafuta ipo Sudan, marekani hawezi hangaika tangu 1970s kuigawa Sudan Kisha aiache kwa mchina
 
Sudan haina mamlaka ya kueleweka kwa sasa hivyo hakuna udhibiti wa mafuta, kama China hawaingilii wangeondoka mpaka kuwepo na serikali yenye udhibiti wa nchi.
China haingiilii mamlaka za Nchi
 
Rapid Support Forces(RSF) walioanzisha mapigano wanafadhiliwa na Russia.
Ukishasema china ana maslahi Sudan sharti umuweke marekani kwenye equation,kugawanywa Sudan ni kazi ya marekani,mafuta mengi yapo Sudan kusini miundombinu ya kuyanywa hayo mafuta ipo Sudan, marekani hawezi hangaika tangu 1970s kuigawa Sudan Kisha aiache kwa mchina
 
China haingiliagi mambo ya uendeshaji wa nchi au utamaduni. Hajikitagi na hayo mambo
 
China haingiliagi mambo ya uendeshaji wa nchi au utamaduni. Hajikitagi na hayo mambo
Unaposema haiingilii inamaanishaje?

Unajua technology tools zinazotumika kuingilia na kubadilisha chaguzi za nchi tofautitofauti zinazotumia na China ili ziendane na matakwa yao?
 
Acha yauwane,halafu wanaume wakiisha sie tutaenda kuoa dada zao na mama zao.
 
Back
Top Bottom