Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,498
- 37,792
Muda wa kawaida wa mchezo umetajwa katika sheria za FIFA kuwa ni dakika 90. Sheria No.7 Kati ya sheria 17 za soka imeelezea vema Muda wa mchezo.
Kanuni zinazotumika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia huko Qatar kuhusu Muda wa mchezo zimekuja kuondoa Tabia ya makipa na Wachezaji kujilaza chini bila sababu Kwa Muda mrefu kisha Muda huo kutofidiwa kikamilifu na hivyo kufanya baadhi ya Mechi zichezwe Kwa dakika 80 badala ya 90 huku Muda mrefu ukipotezwa na wachezaji hususan Makipa. Kanuni hii ikitumika kwenye ligi ya NBC itawasaidia Metacha Mnata wa SBS na Dida wa Namungo kubadilika na kuacha mpira utembee badala ya kujilazalaza.
Kombe la Dunia ukilala wewe lala lakini ujue Hakuna dakika itakayopotea bure. Refa ataongeza dakika zote ulizopoteza. Tangu Mechi ya ufunguzi Jana Kati ya mwenyeji Qatar na Ecuador, na ya Leo Kati ya England na Iran dakika zingionhezwa chache ni 5.
Leo England Vs Iran kipindi cha Kwanza zimeongezwa dakika 14 na kipindi cha pili zimeongezwa dakika 10. Yaani dakika za nyongeza Kwa Mechi nzima ni 24 ambazo ni zaidi ya nusu ya kipindi kimoja.
Hii ndo komesha ya wapoteza Muda Kwa makusudi.