Fikra Angavu
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 301
- 105
Habari zenu wadau JF
Tanzania ni moja ya nchi ambayo wananchi wake hawana uelewa Mkubwa juu ya sheria zinazo tuzunguka.. zinazotutawala...
Kuanzia sheria/haki za kibinadamu hadi sheria zinazotusimamia sisi kama raia na haki zetu.
Tatizo lipo wapi...!?
Kuna pande mbili.
Inaweza ikawa sisi kama raia hatujitumi/hatujishughulishi kujua hizi sheria na haki zetu
Au
Serikali haijatafuta njia rahisi za kuwapelekea wananchi wake kufatilia sheria hizo au kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu na faida za kujua sheria zinazo tuzunguka.
Kuna haja ya serikali kuandaa mikakati ambayo itawawezesha wananchi kujua sheria na kupunguza mzigo wa kutumia nguvu nyingi katika kuwaelewesha raia.
(Ruksa kunikosoa.. maana tupo kujifunza)
1. Serikali/mahakama isambaze elimu kwa raia wake kuhusu umuhimu wa kujua sheria na katiba ili kutambua haki zao.
2. Iandae vipindi vya redio na tv vya kila wiki ili kuwaeleza/kuwatafsiria sheria zinazotuzunguka na umuhimu wake.
3. Iingie ubia na mitandao ya simu kuandaa namba maalumu za kutuma jumbe mbali mbali zinazoelezea sheria na haki za raia katika nchi.. kwa malipo madogo au bure ili wengi waweze kufatilia (wanauchumi wataongezea)
4. Serikali ifungue tovuti ya sheria na katiba.. itakayokua inaelezea sheria, tafsiri zake pamoja na haki za raia wake (uhusiano wa hivi vyote)...
5. Kuna vijana wengi sana wanaosomea sheria wanabaki mtaani.. watumike katika kusambaza elimu mitaani au kwa viongozi wa serikali za mitaa ili iwe rahisi kwa wao kuenezeana elimu hio kwa raia wake.
Yakifanyika haya.. watu wakajua sheria, haki zao pamoja na katiba....
Itaongeza hari ya uzalendo, umoja na jamii inayotambua uwepo wao kama raia wa tanzania....
Ni upeo wangu umefikia hapo... unaweza kunipinga kwa hoja lakini pia kuni unga mkono kwa hoja vile vile