Sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto ambaye wazazi wake wameachana?

loupa

Senior Member
Jul 22, 2016
121
72
Ndugu wana Jf Mimi ni kijana wa miaka 26 nilioa binti mmoja miaka 3 iliyopita tukabahatika kupata mtoto mmoja.

Maisha yetu yakaleta mgogoro mkubwa mwaka mzima sasa.

Nikaamua kumuacha, nilipokuwa namkabidhi Yule mwanamke wazazi wake walinitaka kutoa matunzo ya mtoto Kwa tsh 200,000 kila mwezi.

Sasa nikajiuliza kama sina inakuaje? Na kama akipata shida ya kuzidi gharama ya hiyo pesa itakuwaje? Japo Kama suala la matibabu bima nishamkatia!

Suala jingine
Kama hujafunga ndoa na huna cheti cha NDOA name mwanamke mnagawana mali mlizonazo au Sheria ikoje kuhusu hili

Naomba Masada hapo.
 
Kwanza, uliishi na huyo mama kwa miaka 3 kwa maelezo yako kwahiyo kisheria HUYO NI MKEO.

Pili, matunzo ya mtoto hayana fixed rate kwa kila mtu. Inategemea baba unapata shilingi ngapi. Kama mnashindwa kabisa kukaa mkapangiana wenyewe pelekaneni ustawi wa jamii alafu hao wazazi na mtoto wao watatakiwa ku justify kwanini wamesema laki 2 na wewe utatakiwa kusema unatoa ngapi na kwanini.

Tatu, kwa ushauri wangu, achana na wazazi wa mkeo, kaa chini wewe na mzazi mwenzio wekeni hasira pembeni na msikomoane ila pangeni namna bora ya kumtunza mtoto. Kwani nikuulize mkuu, baada ya kuachana hautapenda kuona mtoto wako anaishi vizuri? Najua jibu ni ndio na hapa shida inakuwaga kina mama wanataka ikiwezekana wachukue mshahara wako wote umtunze mtoto na yeye mwenyewe ikiwezekana hata ukija kupata mwanamke mwingine asineemeke na mshshara wako.

Nne na mwisho, kuachana liwe suluhisho la mwisho kabisa. Gharama ya kuachana huwa ni kubwa sana. Kwako, Kwake mama mtoto na kwa mtoto pia!
 
Back
Top Bottom