Sheria inasemaje kuhusu haya?

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Ni matumaini yangu kuwa nimelileta hili swala huku nikiamini ntapata ufafanuzi wa kisheria kuhusu utata uliojiri Arusha na kupelekea kutokea fujo zilizosababisha vifo.

Kwanza, naomba kueleweshwa juu ya uhalali wa diwani Chitanda, je sheria na taratibu zinasemaje kuhusu madiwani wa viti maalum?, mbona akina owenyo walipigia hai?

Pili, je sheria zinasemaje iwapo wajumbe wengine watasusia uchaguzi wa halmashauri, hapa namaanisha ni idadi gani inaruhusiwa kuendelea na uchaguzi hata kama wengine hawapo?.

Tatu, je nihalali polisi kuzuia mkutano au maandamano kisheria iwapo kutokana na vigezo vyao wataona kunahitaji la kufanya hivyo?

Nne, je ni halali kiongozi wa kisiasa kuamrisha wafuasi wake kwenda kituoni kuwachukua waliokamatwa?.

Ninaomba tafadhali tulijadili kisheria zaidi na si kisiasa kama linavyo jadiliwa ktk majukwaa ya siasa. naamini hii iatatusaidia wengi kujua sababu ya mkasa mzima uliojiri.
Nawasilisha
 
Kwa swali lako la kwanza huyu apa msajili wa vyama vya siasa na ufafanuzi wa kisheria, namnukuu.

Anasema ufafanuzi walioupata juu ya uhalali wa wabunge hao wa viti maalum waliokuwa wakilalamikiwa na vyama vyote viwili ni kwamba, sheria inawatambua wabunge kama madiwani wa sehemu wanazotoka na inaendelea kufafanua chama kinachowakilishwa na mbunge wa viti maalum, kitakuwa na haki ya kumpangia kazi sehemu yoyote isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo lingine.


 
Nashukuru kwa jitihada zako, ingawa naona kama bado sijashiba na jibu hilo
 
Back
Top Bottom