Sherehe za Ushindi wa CCM jimbo la Kalenga.

Sherehe za Ushindi wa CCM jimbo la Kalenga.

HONGERA CCM KWA KUKOKOTA WATANZANIA WASIOJIELEWA,KUNAHAJA YA KUANZISHA KAMPENI MAALUMU YA KUWAZINDUA WOOTE WALiO WALALAFI!
 
Naungana na ccm iendelee kuwanyonya damu wajinga kama kupe, majimbo kama haya ndio ninapopata hoja isiyo na mashiko eti wanawake wanataka 50 kwa 50 hii haikubaliki kamwe kwa sababu hata wanawake wanapopewa fursa hawaitumii badala yake wanaomba hisani kwa mabazazi.
 
Ukiangalia picha hii utaona kuwa watu wa Kalenga hawakuwa na mpango na huyu Lema......
lma.jpg
 
Kila mwananch ana hak ya kuchagua kiongoz ampendae, mwenye sera zinazomridhisha! Sasa haya mambo ya wakosaji kuanza kuwatukana wana kalenga kuwa hawana akil Yanatoka wap!!
Hongeren CCM

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums

Ndiyo maana wanapuuzwa kama hivi.....
View attachment 145270
 
Siasa za maji taka kama zito alivyosema ndo zinawaponza... wananchi wamefanya uamzi sahihi.
 
Safi sana wala Kalenga mmenifurahisha bado Ridhiwan afanye yake Chalinze hiyo ni salam ya 2015
 
Hongereni Magamba. Ujinga wa wana-kalenga umekuwa mtaji wenu wa ushindi.

Hapana sio Ujinga tu, supporter wengi wa Chadema hawakupiga kula kwani NEC haitaki ku-update daftari la kura. Na sababu kubwa ni hizi chaguzi ndogo.
 
Watu walio wengi wa jimbo la kalenga hawajitambui kabisa yaani ni negative digit kichwani mwao

Ni haki yao kupiga kura watakavyo kwa wanayeona anafaa na hiyo ndio democracy and nothing else.
 
Hongereni Wapinzani (CCM), ila kuna kambinu mmetumia sio hivi hivi.

Hongereni sana ila kama wakubwa wetu tunawaombeni msiweke vikwazo kwenye maboresho ya Daftari la wapiga kura.

Hongereni Ufalme wa CCM, Baba hadi Mtoto.
 
hawakupiga kura kuchagua mtu bali walichagua chama hawa..kuiondoa ccm vijijini inahitajika nguvu ya ziada kwa wapinzani na kwa mtindo huu kuishika nchi itakua ndoto kwani watu wengi sana bado hawajajitambua na.wanaona ccm ndo kila kitu...inabidi wapinzani hasa chadema wabuni mbinu nyingine za.kuwaelewesha wananchi hasa wa vijijini waelewe..kama janja ilotumiwa na ccm kwenye kampeni..nilimsikia Nchemba na Mgimwa wakiwauliza wananchi..nanukuu" Kalenga mna shida ya majiiii wananchi..ndiyooo!! mlishawahi kuona waziri wa maji wa chademaaaa??? wananchi..hapanaaa!!hata ofis hatujui zilipo..wananchi mlishawahi kuona waziri wa afya wa chadema?? hapanaaa..mwisho wa kunukuu..
ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wananchi kuliwafanya ccm watumie mwaya huo kuwapumbaza bila kuelewa kuwa hata hayo maji hawawezi kuyapata direct kutoka kwa huyo waziri bila watu wa chini yake kama mbunge ama diwani..kwanino hawakuwauliza kama wamewahi kuona mbunge ama diwani wa.chadema?
Chadema msiweke nguvu majimbo ya mjini tuu..vijijini ndipo watu walipo wengi..tafuteni njia ya kwenda na hawa watu polepole..mnavyofanya sasa ni sawa na profesor afundishe mwanafunzi wa chekechea..nendeni nao polepole kulingana na uwezo wao kuelewa mambo..sasa mkiwaambia kuna mabilion yamefichwa uswiz hapo watawaelewa kweli..mwingine anaweza kusema bilioni ni kitu gani na uswiz ni wapi? sipo kiitikadi hapa nimeandika kama mwananchi wa kawaida kwani sina kadi ya ccm wala chadema wala cuf..so mimi ni mwananchi huru..
 
Back
Top Bottom